| E-mail this to a friend | Printable version |
|
||||||
| Session No | Question Number | To the Ministry of | Sector | Date Asked | ||
|---|---|---|---|---|---|---|
| 8 | 109 | REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT | Local Government | 2 July 2012 | ||
| Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Nianze kwa ku-declare interest kwamba mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii, sasa swali. Mheshimiwa Mwenyekiti, katika shule nyingi ambazo tumepita kuna uhaba mkubwa sana wa walimu wa taaluma hususani kuhudumia watu wenye ulemavu. Serikali ina mpango gani wa kuongeza idadi ya walimu hawa? |
||||||
| ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 109 SESSION # 8 | ||||||
|
||||||
| NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Dkt. Mbassa kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, tumezungumza na watu wa kitengo hiki mara tu baada ya kupata hili swali. Tumshukuru sana Mheshimiwa Kwegyir ambaye anafuatilia sana masuala ya walemavu. Kila wakati tumekuwa na utaratibu wa kuhakikisha kwamba walimu hawa wanaongezeka na idadi yao inaongezeka. Sina takwimu hapa kwamba ni kiasi gani tumefanya katika hilo eneo na niombe tu kumthibitishia kwamba kila wakati idadi hii imekuwa inaongezeka, wengine wako katika shule wanafundisha, lakini anaamua kwenda Chuo Kikuu ili kwenda kujifunza mafunzo maalum kwa ajili ya walemavu. Mimi mwenyewe nimejifunza habari hii, mwalimu wangu pale Chuo Kikuu Dkt. Gichoi ndiyo alikuwa anafundisha, nafikiri siku hizi wanamwita Dkt. Mboya. Ametufundisha eneo hili kwa hiyo, nalifahamu jambo analolizungumza hapa. Lakini idadi yao imekuwa inaongezeka kutokana na mahitaji haya ya nchi kwa ujumla. Baadaye nitamtafutia takwimu ili kuweza kuona jinsi ambavyo imekuwa inapanuka. |
||||||