You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Supplementary Question

mp Mallole, Dr. David Mciwa[CCM]

Dodoma Mjini Constituency
Session No Question Number To the Ministry of Sector Date Asked
8 100 WORKS Transport/Road 29 June 2012
Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana na naomba kuuliza maswali madogo mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza. Nashukuru kwa kazi nzuri ambayo Serikali inaendelea kuifanya ya
kukarabati barabara hiyo ili iendelee kupitika wakati wowote. Je, ni lini sasa Serikali itajipanga kuitengeneza barabara hiyo kwa kiwango cha lami kwa kuzingatia kwamba Chuo cha Serikali za Mitaa cha Hombolo ndio Chuo Kikuu pekee kilichopo katika nchi yetu ya hapa Tanzania.

Pili, nimeenda mwendo wa kasi sana kukagua barabara tunazokwenda Dodoma/Iringa na Dodoma/Babati na kwa kweli kazi inaendelea vizuri na bila shaka lami itaingia hapa mjini kwa muda ambao sio mrefu kuanzia sasa.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuweza kuona kwamba wakati barabara ya Iringa/Dodoma itakapoingia hapa basi muweze pia kufikisha lami
kwenye Chuo Kikuu cha Saint John’s ambacho kiko
karibu sana na barabara hiyo? Kwa upande pia wa
Kaskazini kwa barabara inayotoka Babati kuingia hapa Dodoma Je, Serikali pia ina mpango gani kuweza kuona kwamba mnafikisha lami kwenye Chuo cha Mipango, Chuo cha Ufundi John Bosco na Chuo cha Madini ambavyo vyote viko karibu sana na barabara hiyo?
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION #  100  SESSION #  8
mp Answer From Hon.Magufuli, Dr. John Pombe Joseph
WORKS
WAZIRI WA UJENZI:

Mheshimiwa Spika, kwanza nampongeza kwa kuishukuru Serikali kwa waliyofanya.

Ninachotaka tu kujibu hapa kwa Mheshimiwa Mbunge
kupanga ni kuamua. Kwa sasa hivi katika mkoa wa
Dodoma Trunk road zote zinajengwa kwa kiwango cha lami. Ukitoka Dodoma hadi Iringa kuna wakandarasi wanatengeneza kwa kiwango cha lami na Dodoma kwenda Singida nayo inajengwa kwa kiwango cha lami na katika Bajeti ya mwaka huu kuna zaidi ya
shilingi bilioni 62 na kitu zimepangwa.

Sasa wakati tukiendelea kujenga barabara za lami
za Dodoma ni lazima Mheshimia Malolle ajue kwamba
kuna maeneo mengi ya Tanzania ambayo hayajajengwa kwa kiwango cha lami ikiwepo Mpanda hadi Uvinza, kutoka barabara ya kutoka Masasi hadi Ruvuma hadi Mbambabay na maeneo mengine, ikiwepo pia kutoka Njombe kwenda Makete. Kwa kuzingatia hiyo na kwamba hiyo resources tuliyonayo tutaendelea kujenga barabara zingine za trunk road hizi za kwenda kwenye Vyuo Vikuu vya Dodoma visubiri mpaka tutakapomaliza kujenga barabara zingine katika nchi hii.