You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Supplementary Question

mp Mwatuka, Clara Diana[CUF]

Special Seat
Session No Question Number To the Ministry of Sector Date Asked
9 113 AGRICULTURE, FOOD SECURITY AND CO-OPERATIVES Food/Agriculture 9 November 2012
Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi na mimi niulize swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa, tatizo la tumbaku nchini linafanana na tatizo la watu wa korosho Kusini, ambalo msimu wake huwa unasuasua na hauna uhakika. Msimu wa mwaka jana 2011 kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani, korosho zilinunuliwa kwa bei ya 1,200/= lakini walilipwa 800/= na zingine kwamba, watalipwa awamu ya pili. Lakini kwa bahati mbaya, awamu ya pili hiyo mpaka leo wengine hawajapata.

Mheshimiwa Spika, sasa msimu uliofuata huu tulionao, kwanza umecheleweshwa. Halafu hivi sasa kuanzia jana wameanza kupata pesa, lakini bei ni ileile ya mwaka jana 1,200/=. Lakini wanalipwa 600/= Mikoa yote miwili na sijui sehemu nyingine, lakini Mtwara na Lindi, wanalipwa 600/= katika 1,200.

Mheshimiwa Spika, sasa kama mwaka jana?

? na mwaka huu si itakuwa hivyo hivyo? Kama ni hivyo, si kuwaibia kiujanja wakulima?

Mheshimiwa Spika, ahsante sana.
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION #  113  SESSION #  9
mp Answer From Hon.Malima, Adam Kighoma Ali
AGRICULTURE, FOOD SECURITY AND CO-OPERATIVES
NAIBU WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA:

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwa ufupi tu. Tatizo la tumbaku na la korosho halifanani sana. Tatizo linalotokana na korosho linatokana na kwamba, mabenki yalipokopesha vyama vya msingi kwenye korosho, ulipaji ule ulikuwa na matatizo.

Tumekwenda tumefanya ukaguzi Mkoa wa Pwani, tutafanya ukaguzi Mkoa wa Mtwara, kwa hivi sasa kinachoonekana ni kwamba, vyama vya msingi viongozi wake wenyewe ndio waliofanya uharibifu ule ambao sasa unazuwia mabenki mwaka huu kukopesha zile fedha. Kwa sababu, benki haiwezi ikaendelea kukukopesha kama hujalipa deni la mwaka jana.

Mheshimiwa Spika, tulichofanya ni kwamba, Serikali, imeyaomba mabenki haya. Tumekutananayo yote. Bei ya msingi ya 1,200/= tunachofanya ni kwamba, itatoka ile asilimia 50%. Vyama vya msingi na vyama vingine vitaendelea kulipa yale madeni yaliyokuwa yanatoka mwaka jana kwa mauzo ya mwaka huu. Italipwa ile; hata usitikise kichwa, ukikopa ni lazima urejeshe.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba niwaambie tu na niwasihi wakulima wa korosho kama ilivyo kwa wakulima wa tumbaku; jamani, vyama vya msingi ni mali yenu na wale viongozi mnawachagua wenyewe. Wakifanya uharibifu, ninyi muwe wa kwanza kuwawajibisha, msisubiri Serikali.