You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Supplementary Question

mp Robert, Rachel Mashishanga[CHADEMA]

Special Seat
Session No Question Number To the Ministry of Sector Date Asked
4 344 AGRICULTURE, FOOD SECURITY AND CO-OPERATIVES Irrigation 1 August 2011
Mheshimiwa Spika, ahsante. Ninataka kuuliza swali dogo la nyongeza kama ifuatavyo:-

Kwa kuwa Manispaa ya Shinyanga imekuwa ikikumbwa na ukame mkubwa hasa kipindi cha mwaka wa 2011; na kwa kuwa mito na mifereji hiyo imekuwa ikisubiria mvua ndiyo ijae; je, Serikali haioni sasa baada ya Miradi hiyo kukamilika itumie maji yanayotoka Ziwa Victoria ambayo sasa hivi tayari yako Mkoa wa Shinyanga?
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION #  344  SESSION #  4
mp Answer From Hon.Chiza, Eng. Christopher Kajoro
AGRICULTURE, FOOD SECURITY AND CO-OPERATIVES
NAIBU WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA:

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, labda niseme ushauri wa Mheshimiwa Mbunge tumeuchukua, lengo ni kutumia kila rasilimali tuliyonayo, lakini hizi rasilimali unajua tunapozitumia lazima pia tuangalie ni wakati gani tunatumia, ni kiasi gani na wakati mwingine ni lazima tushirikiane hasa maji ni rasilimali shirikishi.
Mheshimiwa Spika, ushauri wake ni mzuri, tutajaribu kuuzingatia.