Home » Members »Supplementary Question
Supplementary Question
 |
Robert, Rachel Mashishanga[CHADEMA]
Special Seat |
|
|
|
|
|
|
| 11 |
11 |
REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT |
Local Government |
10 April 2013 |
Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Kishapu kuna Mgodi wa Almasi wa Mwadui na inatia aibu sana kuona Hospitali ya Wilaya mpaka sasa hivi haijakamilika.
Je, Serikali haioni kuwa kuna umuhimu wa kukaa na wale wenye Mgodi ili waweze kusaidia kujenga Hospitali hiyo?
|
| ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 11
SESSION # 11 |
 |
Answer From Hon.Majaliwa, Kassim Majaliwa
REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT |
|
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU):
Mheshimiwa Spika, ni kweli kuwa tumetambua kuwa Hospitali yake na Hospitali zingine zina matatizo ambayo pia yanahitaji kuboreshwa na kuchangiwa na wadau ikiwemo wadau hao walioko pale pale Kishapu. Kwa hiyo tunachofanya sasa ni kufanya mazungumzo nao lakini ninaisihi Halmashauri kuanza mazungumzo hayo kwa ngazi yao na pale ambapo wanaona kuna haja ya kuongeza nguvu kutoka ngazi ya Wizara basi tutaungana nao ili kuweza kutoa msukumo wa Wadau hao kuchangia sekta hizo mbalimbali ikiwamo na sekta ya Afya. |
|
|
|