| E-mail this to a friend | Printable version |
|
||||||
| Session No | Question Number | To the Ministry of | Sector | Date Asked | ||
|---|---|---|---|---|---|---|
| 10 | 100 | WATER | Water | 7 February 2013 | ||
| Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Nashukuru kwa majibu ya Naibu Waziri lakini nilikuwa na maswali mawili ya nyongeza. Taarifa nilizonazo mimi ni kwamba hakuna ruzuku inayokwenda KASHWASA na kama inakwenda nilikuwa nataka nijue ni shilingi ngapi inakwenda kwa ajili ya KASHWASA? Mheshimiwa Spika, swali la pili. Kwa kuwa mamlaka mbili Serikali imeona hauna mapungufu. Lakini mimi nasema una mapungufu kwa sababu mpaka sasa hivi ninavyozungumza Mkurugenzi wa SHUWASA amesimamishwa kazi kwa sababu ya ubadhirifu wa pesa. Nilikuwa nataka kujua Serikali haioni kuna haja tena ya ku- review haya mamlaka mbili ili uone ufanisi wake kama ni mzuri au haufai kwa wananchi kwa sababu mtumiaji wa mwisho ndiye anayepata shida? |
||||||
| ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 100 SESSION # 10 | ||||||
|
||||||
| NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, taarifa kwamba anazo taarifa kwamba hakuna fedha zinazopelekwa KASHWASA naomba baada ya kikao hiki nimthibitishie hizo takwimu ninazo na sisi tumekuwa tunatoa ruzuku na ndiyo maana bei ambayo wanalipa wananchi pale iko chini ikilinganishwa na hali halisi ya uwekezaji uliopo kwenye mamlaka hiyo ya KASHWASA. Kwa hiyo, ruzuku inatolewa kwenye sehemu ya umeme na kwa sababu kuendesha umeme ni ghali sana na wakati mwingine mitambo huwa inafungwa kama ukifuatilia ni kwa sababu anadaiwa bill za umeme na inapotokea inabidi Wizara yetu iingilie kati na kupeleka fedha mapema. Kwa sasa hivi kwa taarifa tuliyo nayo madeni makubwa ambayo tunadaiwa kwenye hizi Mamlaka za maji za miradi ya kitaifa ikiwemo hii ya KASHWASA, ikiwemo ya Makonde na mingine mingi ambayo madeni makubwa kwa sababu gharama za uendeshaji ni kubwa na hasa kwa upande wa umeme. Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la pili kwamba muundo uliopo yeye anaamini hautoshelezi mahitaji na ana taarifa kwamba Mkurugenzi amesimamishwa kazi. Labda nitoe ufafanuzi kwamba yule Mkurugenzi hakusimamishwa na KASHWASA Mamlaka ya Maji ya Shinyanga na yale ni maamuzi ya Bodi. Kwa hiyo, Mwenyekiti na Bodi yake baada ya kubaini kwamba huyu Mkurugenzi ana mapungufu ya ubadhirifu kama tulivyo na taarifa wamemsimamisha kazi na ni haki yao kufanya vile kwa sababu wamepewa mamlaka hayo na Waziri wa Maji. Kwa hiyo, wamefanya kazi yao vizuri. Lakini hiyo ya kumsimamisha mtu kwa sababu ya ubadhirifu haina maana kwamba mfumo ule sasa una mapungufu. Nadhani ndiyo inafanya kazi vizuri kwa sababu ndiyo mgawanyo wa majukumu waliyo nayo pale. Naomba nirudie kwamba jukumu la KASHWASA ni kusimamia na kuuza maji kwa jumla na ieleweke kwamba sasa hivi tunao mpango wa kupeleka maji Igunga Nzega na Tabora. Kwa hiyo, Mamlaka hii itakuwa na jukumu kubwa huwezi ukaipa tena jukumu la kufanya kazi ya usambazaji. Kazi ya usambazaji kwa wananchi itafanywa na Mamlaka za Maji za Miji husika kama ilivyo SHUWASA, KUWASA na miji mingine. Ahsante sana. |
||||||