You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Supplementary Question

Session No Question Number To the Ministry of Sector Date Asked
3 100 REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT Local Government 15 April 2011
Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kuniona. Kwa kuwa ni jana tu nimepata taarifa kwamba, Serikali imeanza kufanya utaratibu wa kuwalipa kwa kuwapelekea Wananchi fomu za kujaza, lakini vilevile kwa kuwa wamesema kwamba, wanalipa kwa square meter moja shilingi 750 halafu Serikali itawauzia kwa shilingi 6,000:-

(a) Je, Serikali haioni kwamba haiwatendei haki?

(b) Watu hawa ni wale ambao walihamishwa enzi zile za Mwalimu Nyerere kupelekwa Gezaulole na Kimbiji; sasa wanapoondolewa pale wanapelekwa wapi?
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION #  100  SESSION #  3
mp Answer From Hon.Majaliwa, Kassim Majaliwa
REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU):

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, ninaomba kujibu swali la nyongeza lililoulizwa na Mheshimiwa Philipa Mturano, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, suala la kulipa fedha kidogo katika Halmashauri linao utaratibu wa kisheria kwamba, kwanza, inathaminiwa sehemu ya ardhi inayochukuliwa na thamani ni ile ile ambayo imeandaliwa kiserikali; haina matatizo na wala haina shida katika hilo. Kama kumetokea tatizo la kulipwa fedha kidogo, hilo litakuwa ni kosa lililotendwa na Watendaji wetu pale. Kwa hiyo, ninaweza kuahidi kwamba, nitalifuatilia hilo ili kuweza kutoa majibu yaliyo sahihi.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, Serikali inapotaka kuchukua ardhi eneo ambalo inataka litumike au kwa kupanua maeneo ya miji au kuliendeleza kwa shughuli nyingine ya uwekezaji au vinginevyo; hatua ya kwanza ni kwamba, inakutana na Wananchi waliokaa kwenye eneo hilo kuzungumza nao ili kuweza kukubaliana na hatua utakapotangaza hatua zote za kiserikali, baadaye Serikali inatoa tangazo la kuonesha nia ya kuchukua eneo hilo. Kwa hiyo, eneo hilo linapotaka kuchukuliwa lazima kuwe na mawasiliano kati ya Serikali na Wananchi walioko pale na ni lazima waridhie na wakisharidhia, taratibu za kawaida za uthamini wa eneo hilo zinafanyika na baada ya uthamini, taratibu za malipo zinakamilishwa.