You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Supplementary Question

mp Abama, Mwanamrisho Taratibu Maalim[CHADEMA]

Special Seat
Session No Question Number To the Ministry of Sector Date Asked
4 14 VICE PRESIDENT'S OFFICE (UNION AFFAIRS) Union Affairs 8 June 2011
Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Waziri naomba nimwulize suala moja la nyongeza.

Kwa kuwa utaratibu wa mgao mpya wa mapato ndio kwanza unataka kuanza au unasubiri maamuzi ya Serikali zote mbili. Je, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa kauli gani kuhusu kufidia siku ambazo Serikali ya Zanzibar imekosa mgao huo?
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION #  14  SESSION #  4
mp Answer From Hon.Suluhu, Samia Hassan
VICE PRESIDENT'S OFFICE (UNION AFFAIRS)
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO):

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema awali kwamba Serikali zetu mbili ziko katika kujadiliana kuhusu mgao wa fedha hizo. Katika majadiliano hayo kama suala la fidia litakuja basi nalo litajadiliwa na wataafikiana ipasavyo. Ahsante sana.