You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Supplementary Question

mp Matiko, Esther Nicholas[CHADEMA]

Special Seat
Session No Question Number To the Ministry of Sector Date Asked
11 107 WATER Water 25 April 2013
Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Licha ya kwamba Mkoa wa Mara tumezungukwa na vyanzo vingi vya maji, lakini wananchi wa Mkoa ule hasa akinamama tumeendelea kuteseka kwa kukosa maji.

Katika majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri anaainisha kwamba upembuzi yakinifu ulikamilika mwaka 2010 na anakwenda mbali kwa kusema kwamba watatekeleza kuchimba hilo bwawa la Kanyisambo wakishapata hela. Lakini mbaya zaidi anaainisha visima vinne ambavyo vimechimbwa kwenye Kijiji cha Nyamkonge bila kuzingatia umbali kijiografia kwa wakazi wa Kata ya Nyahongo.

Mheshimiwa Spika, napenda kujua ni lini sasa Serikali itaipa kipaumbele Kata hii ya Nyahongo na kuchimba hilo bwawa la Kanyisambo ili kupunguza adha ya maji kwa wananchi wa hii Kata?

La pili, wananchi wa Tarime wamekuwa wakiendelea kupata adha kubwa ya maji. Kwa mfano, Tarafa ya Inchugu yenye Kata ya Susuni, Mwema, Sirari na Nyamaraga, tangu tumepata uhuru hatujawahi kuchimbiwa hata bwawa moja. Napenda kujua ni lini Serikali itawapa kipaumbele wananchi wa Tarime kama ilivyo kwingine Tanzania ili na sisi tuweze kupata hilo bwawa?
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION #  107  SESSION #  11
mp Answer From Hon.Mahenge, Dr. Binilith Satano
WATER
NAIBU WAZIRI WA MAJI:

Mheshimiwa Spika, naomba Mheshimiwa Mbunge akubaliane na mimi kwamba Serikali imefanya mambo makubwa sana katika Mkoa wa Mara hasa katika Mikoa ya Ziwa Victoria kwa kuweka miradi mikubwa. Sasa hivi tuna miradi mikubwa ambayo inajengwa pale Musoma kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa Musoma maji.

Mheshimiwa Spika, tunao mradi mkubwa utakaojengwa kutoka Misungwi kwenda Magu na Bariadi kwa kutumia chanzo cha Ziwa Victoria; tunao mradi mkubwa wa kupanua mtandao wa maji Ziwa Victoria kwenda katika maeneo ya Vijijini milimani kama Ilemela; na tunao mradi mkubwa wa kutoa majitaka katika Mji wa Bukoba. Kwa hiyo, Serikali imefanya mambo makubwa. Lakini tatizo hili ni kubwa, nimwahidi kwamba tutaendelea kuweka vipaumbele kulingana na fedha zinazopatikana.

Mheshimiwa Spika, lakini katika Vijiji kumi ambavyo tumekuwa tukivitekeleza, mapendekezo yalianzia kwenye Halmashauri. Kwa hiyo, pale itakapoonekana Kijiji hiki ndiyo muhimu zaidi, basi wao walete mapendekezo, Serikali itakuwa tayari kutoa ushirikiano.