| E-mail this to a friend | Printable version |
|
||||||
| Session No | Question Number | To the Ministry of | Sector | Date Asked | ||
|---|---|---|---|---|---|---|
| 8 | 226 | REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT | Local Government | 20 July 2012 | ||
| Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa Mheshimiwa Waziri ameona umuhimu wa Kamati ya Fedha kushiriki katika Mipango ya Maendeleo na kwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum ni Madiwani. Je, Serikali itaangalia lini utaratibu wa Wabunge wa Viti Maalum kushiriki katika Kamati ya Mipango na Fedha katika maeneo yao kwa kuwa suala hili limekuwa likizungumzwa mara kwa mara na Mheshimiwa Waziri Mkuu alilitolea maelezo kwamba hakuna tatizo. Mheshimiwa Waziri mwenyewe alishawahi kuzungumzia umuhimu huo, lakini utekelezaji wake unasuasua. Ni lini sasa utakamilisha kanuni ili tuweze kushiriki Wabunge wa Viti Maalum katika Kamati ya Mipango na Fedha? |
||||||
| ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 226 SESSION # 8 | ||||||
|
||||||
| NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru sana Mheshimiwa Chiku Abwao kwa kutambua kwamba tuliwahi kulisemea jambo hili. Mimi niliwahi kusimama hapa nikasema nimezaliwa na mama na mke wangu ni mama. Kwa hiyo najua umuhimu na wala hapa sitaki kuzua mgogoro hapa tukaanza kushindana hapa umuhumi wa hawa. Mimi natambua akinamama wana umuhimu mkubwa sana katika taifa. Jana ameondoka Mheshimiwa Rais wa Liberia mwanamama, amekuja hapa tumemwona wote mizinga 21 amepigiwa pale. Kwa hiyo natambua umuhimu wao na Chama changu cha Mapinduzi kinawatambua akinamama. Tulipokuwa tunajibu jambo hili tulisema kabisa kwamba Mbunge huyu wa namna hii kwa sababu ni wa Mkoa walau achague Halmashauri moja ambayo angetaka ashiriki. Kwa sababu hawezi akawa anatoka Rombo, anakwenda Siha anakwenda kule, anakwenda Same pamoja na kwamba anawahudumia wananchi. Ikasemwa kwa uzito mkubwa sana baadaye Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa sababu limekuwa linajitokeza akalibeba yeye mwenyewe. Sasa hebu jiulize Waziri Mkuu na mimi nani mkubwa? Yaani mimi nianze kukataa hapa, Waziri Mkuu alishasema analibeba na mimi nikisema nikujibu kwamba sasa tayari imekuwa, ataniambia bwana mdogo hii habari umeipata wapi. Nataka nithibitishe kwako hapa kwamba jambo hili Mheshimiwa Waziri Mkuu amelichukua kwa uzito mkubwa. Kwa hiyo anaendelea kulifanyiwa kazi, tunaiona hiyo concern na haya mabadiliko ambayo yanatokea na nadhani kwamba tutafika mahali tutalitatua. Kwa hiyo tunakaribisha wazo hili na tunawatambua akinamama. |
||||||