You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Supplementary Question

mp Madabida, Zarina Shamte[CCM]

Special Seat
Session No Question Number To the Ministry of Sector Date Asked
8 297 EDUCATION AND VOCATIONAL TRAINING Education 31 July 2012
Mheshimiwa Spika,
ahsante sana. Nina maswali madogo ya nyongeza.
(a) Kwa kuwa inajulikana kabisa kwamba kuna
shule nyingi sana za watoto wenye ulemavu na Waziri
anashuhudia kwa sababu tumezitembelea hizo shule
na tumewakuta watoto hawa wanahangaika,
ninaomba kujua hivi ni kweli Serikali inayo takwimu ya wanataaluma ambao wamemaliza?

(b) Je, Serikali sasa inawaambia nini hawa watoto ambao wamekuwa wanahangaika wanashinda mchana kutwa bila kufundishwa wakati walimu wapo ambao hawana kazi?
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION #  297  SESSION #  8
mp Answer From Hon.Mulugo, Philipo Augustino
EDUCATION AND VOCATIONAL TRAINING
NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI:

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema kwenye jibu
langu la msingi, takwimu za walimu waliomaliza Vyuo vye Elimu Maalum ambavyo kwa Tanzania nzima
tunavyo Vyuo viwili tu vinavyotoa mafunzo ya Elimu
Maalum.

Kwa Chuo cha Serikali ni chuo cha Arusha chuo
cha Patandi na Shirika la dini wametusaidia kuanzisha chuo pale SECUCO. Hivyo ndiyo vyuo pekee
vinavyotoa mafunzo kwa walimu elimu maalum kwa
Msingi, Sekondari na hata Shahada.

Mheshimiwa Spika, kuhusu takwimu kwa sababu
amehitaji ninazo ofisini nitajaribu kumpatia Mbunge.

Lakini hapa ninayo takwimu tu ya Walimu waliomaliza ambao ni 539 kwa mwaka 2010/2011.

Mheshimiwa Spika, swali la pili juu ya watoto
wanaohangaika hawana walimu. Ni kweli tumejaribu
kulihangaikia hili na ndiyo maana tukalifanyia uharaka wa hali ya juu sana.

Wapo Walimu ambao hawajaajiriwa, Walimu wa
Kawaida lakini kwa wale wa Elimu Maalum tumewajumuisha pamoja kwa miaka yote miwili
2010/11 tumeweza kuwaajiri mwezi huu wa saba na
Wabunge mkienda kwenye tovuti ya Ofisi ya Waziri
Mkuu TAMISEMI inayoshughulikia Elimu Maalum kwa
kushirikiana na Wizara ya Elimu tumeweka tayari
Walimu ambao watasambazwa kwenda kufundisha
kwenye hizo shule za Elimu Maalum.