| E-mail this to a friend | Printable version |
|
||||||
| Session No | Question Number | To the Ministry of | Sector | Date Asked | ||
|---|---|---|---|---|---|---|
| 8 | 269 | WATER | Water | 26 July 2012 | ||
| Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maji, nina maswali mawili ya nyongeza. Serikali kwa kushirikiana na GGM walianzisha mradi wa kutoa maji ziwa Victoria mradi ambao ulikadiriwa kuwa bilioni 15.3, hadi sasa GGM imeshatoa bilioni 6.99. Je, ni lini Serikali itatoa pesa hizo kusudi mradi huu wa maji ukamilike na watu wa Geita tupate maji? Swali la pili, kule Bukombe na sasa ni wilaya nyingine tena inatiwa Mbogwe kuna kituo cha watoto yatima kinaitwa FTI Masumbwe, watoto hao wamekaa katika wakati mgumu hawana maji kwa muda mrefu sana na kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo tulifuatilia tukaomba Serikali itusaidie kichimba kimechimbwa tangu mwaka jana mwezi wanne, na mpaka hivi sasa maji hayajaanza kutoka ina maana kwamba pump haijapelekwa. Nitumie nafasi hii basi kuiomba Serikali kupitia Wizara ya Maji ifungwe pump ili wale watoto waweze kupata maji kwa sababu maji yako mengi sana na lita 5000 kwa saa ni maji yanatosha kabisa kuwasaidia watoto yatima na wanakijiji wa eneo hilo ahsante sana. |
||||||
| ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 269 SESSION # 8 | ||||||
|
||||||
| NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, kwanza nichukue fursa hii kumpongeza sana Mbunge Vicky Kamata na Wabunge wote wa Geita kwa namna wanavyofuatilia katika majimbo yao wilaya nzima ya Geita bila kumsahau Mheshimiwa John Magufuli wa jimbo la Chato. Sasa kuhusu suala GGM, Geita Gold Mine Limited, kwanza tuwashukuru sana kwa msaada wao mkubwa ambao wameutoa wa milioni nne nukta tano dola ambazo ni sawa na six point nine billion hela za Kitanzania. Sasa wao wanatoa maji kutoka kwenye chanzo wanaweka miundombinu na wanayatoa yale maji mpaka kwenye sehemu ambayo itajengwa tenki kwa gharama zao. Serikali iliahidi sasa kutoka pale ambapo wanaweka tenki kupeleka miundombinu kwa watumiaji ambazo ndizo fedha bilioni tisa. Sasa Serikali imeshaongea kwa sababu kuna mradi mwingine sambamba unaoitwa Lake Victoria Watu ambao unafadhiliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki umepata mafanikio makubwa wilaya za Nasiyo, Geita na Sengerema na Geita peke yake ina dola milioni nne nukta mbili nadhani ni kazi ambayo iko chini ya Waziri wa Afrika Mashariki ambaye yuko hapa Mheshimiwa wa Viwango. Kwa hiyo tumekubaliana Serikali kwamba badala ya kuwa na miradi miwili parallel ni vizuri fedha hizi milioni 4.2 ambazo zimepangwa kwa ajili ya Geita zitumike sasa kutoa maji wale watakapoishia wale wafadhili wa GGM kupeleka kwa wananchi kwenye ile miundombinu. Kwa hiyo nadhani hilo litakuwa limetatatuliwa na tushirikiane kuona linatekelezwa. Kuhusu swali la pili kwamba kule Bukombe kuna kituo cha watoto yatima, hakina maji na kisima kimechimbwa pump inatakiwa inunuliwa na iweke iweze ku-pump nataka nimwambie Mheshimiwa Mbunge kwamba Bukombe katika sealing ya fedha za vijiji kumi wanazo zaidi milioni 900 sasa hivi wakiangalia orodha ambayo tulikuwa tumeweka kwenye pigeon hole basi wakae na Halmashauri waweke kipaumbele katika milioni 900 kununua pump ambayo haitazidi milioni 50 kwa ajili ya kituo cha watoto yatima. |
||||||