You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Supplementary Question

mp Changulla, Josephine Tabitha[CCM]

Special Seat
Session No Question Number To the Ministry of Sector Date Asked
7 115 EDUCATION AND VOCATIONAL TRAINING Education 20 April 2012
Mheshimiwa Spika, ahsante.
Pamoja na majibu mazuri kabisa ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba
kumwuliza swali moja la nyongeza kama ifuatavyo:-
Kwa kuwa katika Mkoa wa Kanda ya Ziwa hususani Mkoa mpya wa
Geita tatizo la ukosefu wa mabweni ni kubwa na ni kubwa kweli kweli.

Watoto wetu na hasa watoto wa kike wamekuwa wakipata elimu yao
katika mazingira magumu na hatarishi kweli kweli.
Mheshimiwa Spika, watoto hawa wamekuwa wakilazimika
kupanga kwenye nyumba za watu binafsi na kibaya zaidi wamekuwa
wakipata mimba na magonjwa mbali mbali mabaya kama UKIMWI na
kadhalika.

Je, Serikali haioni kuna haja ya kunusuru maisha ya watoto hawa
kwa kutumia hata Mashirika ya Umma kama vile National Housing
Corporation (NHC) kuweza kujenga mabweni katika shule zetu za
Sekondari?
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION #  115  SESSION #  7
mp Answer From Hon.Mulugo, Philipo Augustino
EDUCATION AND VOCATIONAL TRAINING
NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI:

Mheshimiwa Spika, kama tulivyosema katika awamu ya kwanza, Serikali inayo nia ya
kuendeleza elimu nchini, lakini kikubwa hapa ni ufinyu wa bajeti. Kama
tulivyosema pia kwamba, tumetenga fedha kwenye mpango wa MMES
wa kujenga hosteli 20 at least kwa kila mwaka. Naomba labda
nimweleweshe Mheshimiwa Mbunge jambo moja, tunaposema shule za
bweni na tunaposema kujenga hosteli ni kitu tofauti kabisa. Shule za
bweni maana yake wanafunzi wote kutoka Form One ama mpaka Form
Six maana yake wanakaa shuleni hapo hapo, wavulana au wasichana,
wanakula hapo, wanalala hapo na wanachaguliwa kutoka sehemu
mbalimbali za Tanzania Bara.

Mheshimiwa Spika, hosteli ni nyumba tunazojenga kwa kushirikiana
na Halmashauri ama Baraza la Madiwani kule kwenye Kata, zile Ward C’s,
wanakaa pamoja wanakubaliana kwamba tujenge hosteli kwa ajili ya
watoto wanaokaa mbali na kituo cha shule kilipo, maana wanatoka
kwenye vijiji mbali kidogo. Kwa hiyo, hosteli ni nyumba tu ambayo
tunakuwa tumeweka pale kwa ajili ya wanafunzi wanaotoka mbali lakini
inakuwa ni mchanganyiko, wanafunzi wanaokaa hosteli na wengine
wanatoka mbali. Tunazo shule za mfano huo kama vile Lugalo, Mbeya
Day, hata pale Azania na Tambaza.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kunakuwa na wanafunzi wanatoka
day na wengine wanakaa pale hosteli, lakini shule za bweni ni kwa ajili ya
bweni tu na watoto wanatoka katika different dejects kama vile Songea
Boys, Tabora Boys na shule zingine za mfumo huo. Kwa hiyo, kwa upande
wa Geita, ukosefu wa hosteli, namwomba Mheshimiwa Mbunge kwa
sababu na yeye ni Mjumbe kwenye Halmashauri ya Wilaya, wakae,
wapange, waone ni namna gani wataweza kusaidia.

Lakini bado Serikali
sisi tutachangia mfumo mwingine kama nilivyosema kwamba tutajenga
hosteli 20 na kila mwaka tunaweka bajeti hiyo.