| E-mail this to a friend | Printable version |
|
||||||
| Session No | Question Number | To the Ministry of | Sector | Date Asked | ||
|---|---|---|---|---|---|---|
| 7 | 102 | COMMUNITY DEVELOPMENT, GENDER AND CHILDREN | Projects/Fund | 19 April 2012 | ||
| Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Asasi nyingi zisizokuwa za Kiserikali, zimekuwa zikisaidiana na Serikali katika kutoa elimu katika jamii na kusaidia shughuli za kimaendeleo. Lakini baadhi ya asasi zisizo za Kierikali zimekuwa zikishindwa kufanya hivyo na matokeo yake kujihusisha kwenye masuala ya kisiasa na kujenga chuki kati Serikali na wananchi kwa ajili ya kutimiza azma za kisiasa kwa baadhi ya vyama fulani fulani:- (a) Mheshimiwa Spika, huku tunakoelekea, tunaenda katika mchakato wa Katiba mpya na tuna habari kwamba kuna baadhi ya vyama vimejipanga kuhakikisha kuleta asasi zisizo za Kiserikali kwa ajili ya kushinikiza wananchi kutimiza malengo yao ya kisiasa na agenda zingine katika Katiba mpya. Je, Serikali wanalijua hilo na wamejipanga vipi? (b) Mheshimiwa Spika, kuna malalamiko katika ada ya usajili na kama tunavyojua vijana wengi ambao wanamaliza elimu ya juu mbali ya kwamba kuna tatizo ya ajira, lakini wengi wamekuwa wakipenda kuanzisha NGO zao, lakini wanakwama kwenye ada ya usajili. Je, Serikali haioni kwamba kuna haja ya kupunguza ada hiyo ili vijana wengi waweze kuanzisha NGOs zao? Mheshimiwa Spika, ada yenyewe ni shilingi laki mbili. |
||||||
| ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 102 SESSION # 7 | ||||||
|
||||||
| WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO: Mheshimiwa Spika, naomba kumjibu Mheshimiwa Ester Bulaya, maswali yake mawili ya nyongeza:- Kwanza ningependa niwafahamishe wananchi kwamba kila NGO imeanzishwa ikiwa na majukumu ambayo yamo katika Katiba yake. Kwa hiyo NGO ambazo zinaacha majukumu yake na kufanya majukumu mengine ni uvunjaji wa sheria ambayo imeunda ile NGO. Wizara yangu kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la NGO iliandaa Kanuni za madili za NGO ambayo ilipitishwa 2008. Kwa hiyo, hizo NGOs zikiwemo pia na NGO za briefcase zinatakiwa kuchukuliwa hatua:- (a)Mheshimiwa Spika, tuna Maafisa Maendeleo ya Jamii ambao ni wasajili wa NGOs katika kila Wilaya. Kwa hiyo, kwa kupitia Bunge hili nawahamasisha na kuwaagiza wale Maafisa wa Maendeleo ya Jamii katika Wilaya waangalie kwamba NGOs ambazo zinafika katika maeneo yao na kufanya majukumu mbali na yale ambayo yameandikwa watufahamishe ili hatua stahiki zichukuliwe. (b)Swali la pili linazungumzia kuhusu ada ya usajili kuwa ni ya juu. Naona hili pengine tulichukue na tulifanyie kazi. Lakini nadhani ada iliyopo si kubwa kiasi hicho, lakini bado mimi nalichukua tuliangalie pengine inawezekana ni kweli kwa vijana ambao wanaanzisha asasi zao wanashindwa kufanya hivyo. Ahsante sana. |
||||||
| ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 102 SESSION # 7 | ||||||
|
||||||
| test | ||||||