| E-mail this to a friend | Printable version |
| Session No | Question Number | To the Ministry of | Sector | Date Asked | ||
|---|---|---|---|---|---|---|
| 8 | 328 | INFORMATION, CULTURE AND SPORTS | Youth | 6 August 2012 | ||
| Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali moja la nyongeza. Kwa kuwa, fursa nyingi wamekuwa wakizipata vijana wengi walioko mijini, je, Serikali, ina mkakati gani wa kuwafikia vijana walioko vijijini katika uundwaji wa Baraza hili? | ||||||
| ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 328 SESSION # 8 | ||||||
|
||||||
| NAIBU WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO: Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba, inawezekana kuwe na hofu kwamba, vijana wa Vijijini wasipate uelewa juu ya suala hili. Wizara yangu imejipanga kuwaelimisha vijana, kutakuwa na vipindi kuelekea katika kuunda Baraza la Vijana kuanzia katika Television na Redio, ili kupata uelewa. Pia Baraza hili, litakuwa na muundo kuanzia Vijijini hadi Taifa. |
||||||