You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Supplementary Question

Session No Question Number To the Ministry of Sector Date Asked
7 116 AGRICULTURE, FOOD SECURITY AND CO-OPERATIVES Food/Agriculture 20 April 2012
Nashukuru Mheshimiwa Spika, kwa
kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa yapo
malalamiko mengi juu ya suala hili kwa nini isiundwe Tume Maalum kwa
ajili ya kwenda kuchunguza suala hili badala ya kumtuma mtu mmoja
ambaye ni Rais kudanganywa?

Swali la pili, kwa kuwa taarifa hiyo iliyotolewa imeandaliwa na
Halmashauri ya Wilaya ambao ni watuhumiwa wakuu katika suala hili. Je,
Mheshimiwa Waziri yuko tayari kuongozana na mimi mpaka kwa
wananchi hao kwenda kusikiliza kero zinazohusiana na Wizara yake?
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION #  116  SESSION #  7
mp Answer From Hon.Maghembe, Prof. Jumanne Abdallah
AGRICULTURE, FOOD SECURITY AND CO-OPERATIVES
WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA:

Mheshimiwa Spika, sioni
kama kuna sababu ya kuunda Tume Maalum wakati ambapo Mkaguzi
na Mdhibiti Mkuu wa Serikali ameshaandaa ukaguzi maalum katika
jambo hili. Hatua ya kwanza ya ukaguzi huo yaani ile preliminary audit
imeshakamilika na wanajiandaa sasa kwenda kufanya ukaguzi wa pili.

Kwa hiyo, tungoje taarifa yake ili tuweze kuchukua hatua stahiki.

Pili, nitafuatana na Mheshimiwa Mbunge kwa furaha kabisa ili
kusikiliza malalamiko ya wananchi.