You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Supplementary Question

mp Hokororo, Agness Elias[CCM]

Special Seat
Session No Question Number To the Ministry of Sector Date Asked
4 362 HEALTH AND SOCIAL WELFARE Health 3 August 2011
Ahsante Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kunipa nafasi niweze kuuliza maswali ya nyongeza. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, ninapenda kuuliza maswali madogo mawili kama ifuatavyo:-

(i) Kwa kuwa asilimia tatu ya mshahara wanaokatwa wafanyakazi pamoja na ile inayotolewa na waajiri wao ni chanzo kimojawapo katika Mfuko huu wa Bima ya Afya; Serikali haioni kwamba ipo haja ya kuangalia upya marupurupu na mishahara wanayopata Wafanyakazi wa Mfuko kwa kuwa imelalamikiwa kuwa ni mikubwa inatokana na mishahara ya wafanyakazi wetu wa nchi hii?

(ii) Kwa kuwa wataalam wameonesha kwamba kitendo cha kutahiri kinapunguza maambukizo ya UKIMWI kwa asilimia 30; je, kwa nini Mfuko huu usiweke circumcision kama gonjwa mojawapo ambalo linalipiwa na Mfuko kuliko ilivyo sasa kwa kuwataka wanaofanyiwa kitendo cha utahiri kutokulipiwa na Mfuko huu?
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION #  362  SESSION #  4
mp Answer From Hon.Mponda, Dr. Hadji Hussein
HEALTH AND SOCIAL WELFARE
WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII:

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza, ninakubaliana naye kwamba, kuna haja ya kuangalia upya marupurupu ya Wafanyakazi wa Mfuko huu, lakini vilevile tukilenga kuboresha huduma zaidi ambazo wanazitoa. Hiyo ninakubaliana na Mheshimiwa Hokororo, tutaifanyia kazi.

Swali la pili kuhusu tohara kwa wanaume; ni kweli tafiti za kisayansi zimeonesha kwamba, wale ambao wanapata tohara wanapunguza uwezo mkubwa zaidi wa maambukizi ya Virusi vya UKIMWI, ukifananisha na wale ambao hawakupata tohara.

Ninaomba nilitaarifu Bunge lako Tukufu kwamba, Wizara ya Afya tuna mpango kwa Mikoa ambayo ina viwango vya chini vya wanaume waliotahiriwa na vilevile wana viwango vya juu vya
maambukizi ya Virusi vya UKIMWI, tunafanya tohara hiyo bure. Vilevile Mfuko huu nao umeliangalia hili suala na ninaomba nimpe taarifa Mheshimiwa Hokororo kwamba, ni mojawapo ya vitita vilivyoongezwa katika huduma ambazo Mfuko wanatoa pamoja na tohara kwa wanaume.