You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Supplementary Question

mp Hokororo, Agness Elias[CCM]

Special Seat
Session No Question Number To the Ministry of Sector Date Asked
4 105 COMMUNITY DEVELOPMENT, GENDER AND CHILDREN Human Rights 22 June 2011
Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri na mafupi ya Mheshimiwa Waziri, ninapenda kumwuliza maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-

(a) Kwa kuwa Tume ya Nyalali ya Mwaka 1992 ilibainisha kuwa Sheria ya Kimila ya Mirathi inapingana na haki za binadamu; je, Serikali haioni kuwa kwa kuchelewesha kufanya marekebisho ya sheria hizi inavunja baadhi ya vifungu vya Katiba ya nchi?

(b) Sheria ya Mirathi ya Kimila inatumika kwa asilimia 85 ya jamii ya makabila ya Tanzania na imetafsiriwa katika mahakama zote za mwanzo; je, Mheshimiwa Waziri atakubaliana na mimi kwamba ni muda mrefu sasa umepita tangu marekebisho hayo yalalamikiwe na wanawake wengi wa nchi hii; ni lini sasa Serikali italeta hapa Bungeni ili sisi tuweze kupitisha sheria mpya itakayolinda haki za wanawake wajane na watoto?
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION #  105  SESSION #  4
mp Answer From Hon.Mwalimu, Ummy Ally
COMMUNITY DEVELOPMENT, GENDER AND CHILDREN
NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO:

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, ningependa kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Agnes Hokororo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ninakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kwamba, Sheria za Mirathi za Kimila zinazotumika katika nchi yetu, zinabagua kwa kiasi kikubwa wajane na watoto wa kike. Nimfahamishe Mheshimiwa Mbunge kwamba, tuna maamuzi ya mahakama ambapo imetamka kwamba, sheria zote zile, aspect za sheria za kimila ambazo zinapingana na haki za wanawake hazipo operational, tuna maamuzi ya Jaji wa Mahakama Kuu, Jaji Mwalusanya. Kubwa, wakati tunajiandaa kurekebisha sheria hizi, ninaomba nitumie Bunge lako Tukufu kutoa rai kwa Waheshimiwa Wabunge, wahamasishe wanawake na wanaume waandike wosia.

Mheshimiwa Spika, wosia ndiyo njia ya haraka sana itakayowalinda wanawake na watoto wetu wa kike katika mirathi na ninawaomba wanawake hasa walio vijijini, wawabane wanaume kwa sababu experience wenye mali ni wanaume; tuwabane waume zetu waandike mirathi ili tuweze kuwalinda watoto wetu na wake zetu pindi tutakapofariki.

Mheshimiwa Spika, swali la pili ni lini sheria hii italetwa Bungeni; niseme kwamba, Sheria za Kimila zinahitaji mjadala mkubwa sana, kwa sababu zinagusa mila na tamaduni za watu. Kwa hiyo ni lazima Serikali ikusanye maoni kutoka kwa Wadau. Ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali ya CCM ni sikivu, tumeliweka hili katika Ilani yetu ya Uchaguzi na kabla ya mwaka 2015 tutakuwa na Sheria nzuri ya Mirathi, inayolinda haki za wanawake na watoto wa kike. Ninakushukuru sana.