You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Supplementary Question

mp Hokororo, Agness Elias[CCM]

Special Seat
Session No Question Number To the Ministry of Sector Date Asked
3 101 REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT Local Government 15 April 2011
Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, ningependa kumwuliza swali la nyongeza kama ifuatavyo:-

Kwa kuwa Hospitali ya Ndannda ni Teule na inatumika kama Hospitali ya Rufaa kwa Wakazi wa Mkoa wa Mtwara, Lindi na hata Msumbiji na hivyo kusababisha msongamano mkubwa na huduma duni; na kwa kuwa fedha zinazopelekwa katika Halmashauri kwa ajili ya Mpango wa MMAM ni kidogo sana:-

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuongeza fedha katika mpango huo ili kuziwezesha Halmashauri za Wilaya kuharakisha ujenzi wa Vituo vya Afya kama Sera ya Afya inavyoelekeza?
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION #  101  SESSION #  3
mp Answer From Hon.Majaliwa, Kassim Majaliwa
REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU):

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Agness Hokororo, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, suala la kuongeza Vituo vya Afya ni mipango ya Halmashauri yenyewe kwa kuweka kipaumbele kwamba ni vituo vingapi vinahitajika ndani ya wilaya na mtapenda kuanza na ujenzi wa vituo vingapi. Kwa hiyo, Baraza la Madiwani litaweka utaratibu wake. Serikali inapeleka fedha zikiwemo na hizi za Mpango wa MMAM na pia ipo Capitation Development Grant; zote hizo ni zile fedha zinazosaidia kuboresha na kusaidia jitihada za Wananchi walioamua kujenga Vituo vya Afya kadiri ambavyo Baraza la Madiwani limeweka kipaumbele katika ujenzi wa Kituo cha Afya ili kupanua na kuongeza Vituo vya Afya.