Home » Members »Supplementary Question
Supplementary Question
 |
Lwanji, John Paul[CCM]
Manyoni Magharibi Constituency |
|
|
|
|
|
|
| 5 |
12 |
HOME AFFAIRS |
Security |
8 November 2011 |
Mhesimiwa Spika, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza. La kwanza, tumeambiwa hapa tatizo la rasilimali fedha na kwamba, Polisi wamekuwa wakishirikiana na Idara ya Waqnyamapori. Lakini taarifa niliyonayo ni kwamba, eneo lile lilihusisha Chaya, ambayo ni Mbuga ya Uwindaji kwa kushirikiana kwa pamoja na Mbuga ya Hifadhi ya Muhesi Kizigo, huingiza takriban shilingi bilioni 1.9 kwa mwezi, Hazina na eneo hilo ni tajiri na lina rasilimali za kutosha. Je, Serikali haikuona kwamba haikufanya utafiti wa kutosha katika kujibu sehemu ya suala hili?
Mheshimiwa Spika, la pili. Ni kweli kwamba, hutokea magari ya kuja kufanya doria kutoka Manyoni au Singida, lakini hiyo hutokea mara baada ya matukio, lakini kabla ya matukio hakuna gari la aina yoyote na kutoka Itigi mpaka Tabora ni takriban kilometa 300 na vituo hivi ni 12, sasa mpaka litokee tukio ndio wafike. Sasa nadhani kinga ni bora kuliko tiba. Je, bado Serikali haioni kwamba, kuna umuhimu wa kuweka gari katika kituo cha Itigi?
|
| ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 12
SESSION # 5 |
 |
Answer From Hon.Kagasheki, Ambassador Khamis Juma Suedi
HOME AFFAIRS |
|
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI:
Mheshimiwa Spika, masuala haya Mheshimiwa Mbunge Lwanji, rafiki yangu, tumekuwa tunayazungumza sana na nimejitahidi kadri nilivyoweza kukufahamisha Mheshimiwa Mbunge, kwa heshima zote kwamba, tunazingatia umuhimu wa kuhakikisha kwamba usalama unakuwepo katika maeneo husika. Lakini pia kila mara nimekuwa namwambia, endapo rasilimali fedha itaruhusu tutajitahidi kwa kadri tuwezavyo kuhakikisha kwamba tunampatia vitendea kazi kwa wale askari walio katika maeneo haya. Sasa askari wanyamapori ambao tunajaribu kusaidiana nao, hii ni Wizara tofauti na Wizara ya Mambo ya Ndani, lakini bado tuna ule mtandao wa kushirikiana, ila bado hatujafikia kwenye mtandao wa kushirikiana katika rasilimali fedha, lakini tutalitazama hilo.
Mheshimiwa Spika, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge, kuhusu swali lake la pili kwamba, ni kweli wakati mwingine tunajitokeza kwa maana ya Polisi baada ya matukio na sio kabla ya matukio. Lakini hii inaendana na hali halisi ambayo tunayo katika Taifa letu, ambayo ni uhaba wa rasilimali fedha, lakini jitihada kwa kweli zimekuwa zinafanyika na sio kwamba hatuoni umuhimu wa kuweka hivi vituo ama kuweza kumpatia gari Mheshimiwa Mbunge, lakini nataka nimwombe, hili ni suala ambalo tutakuwanalo na tutalizingatia na endapo rasilimali fedha itaruhusu, huko mbele ya safari nimhakikishie kwamba, hilo tutaweza kulitimiza.
|
|
|
|