Home » Members »Supplementary Question
Supplementary Question
 |
Lwanji, John Paul[CCM]
Manyoni Magharibi Constituency |
|
|
|
|
|
|
| 9 |
11 |
COMMUNICATION, SCIENCE AND TECHNOLOGY |
Communication |
30 October 2012 |
Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali mawili madogo, ni mwaka wa tatu sasa toka hii kampuni ilipofanya utafiti na kutoa ahadi ya kuja kuweka mnara pale Mwamageni na mbaya zaidi wenzao wa VODACOM waliweka mnara Mgandu. Halafu wakaendelea wakaruka pale Mwamagembe wakaweka Rungwa na kuwaacha wananchi wa Mwamagembe bila mawasiliano yoyote kwa sababu ya ahadi hii ya hii Kampuni ya Airtel.
Mheshimiwa Spika, mbaya zaidi suala hili sasa limechukua sura ya kisiasa kwa sababu inaonekana kama vile tunatoa ahadi hewa. Sasa ningependa kumwomba Waziri au kumuuliza Waziri anaweza akafunga safari mara baada ya kikao hiki ili twende Mwamagembe ikiwezekana na Afisa wa Airtel kwenda kuwahakikishia wananchi juu ya ahadi hii mpya?
Swali la pili, Mheshimiwa Waziri amesema mwaka wa fedha ujao, lakini ninavyofahamu mwaka wa fedha wa Serikali unatofautiana na miaka ya fedha ya haya makampuni, je, ni lini hasa mwaka wa fedha kwa maana ya mwaka wa fedha wa hii kampuni ya Airtel?
|
| ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 11
SESSION # 9 |
 |
Answer From Hon.Kitwanga, Charles Muhangwa "Mawematatu"
COMMUNICATION, SCIENCE AND TECHNOLOGY |
|
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS:
Mheshimiwa Spika, kama alivyosema kwamba, kweli makampuni yamekuwa yakiahidi, lakini ni vyema vile vile Mbunge akatambua kwamba kutokana na mabadiliko ya kibiashara ahadi hizo zinabadilika mara kwa mara. Lakini nimhakikishie tu kwamba, pamoja na Makampuni haya ya Simu, Serikali kupitia Mfuko wa UCAF, tayari imeshatangaza tenda kwa ajili ya Kata 152 ili kuhakikisha kwamba, mawasiliano yanafika katika maeneo kama hayo. Kuhusu miaka ya fedha ya makampuni haya ni kweli yanatofautiana na mwaka wa fedha wa Kampuni ya Airtel unaoanza tarehe 1 Aprili. Kwa hiyo, ni kuanzia tarehe 1 Aprili, 2013.
|
|
|
|