| E-mail this to a friend | Printable version |
|
||||||
| Session No | Question Number | To the Ministry of | Sector | Date Asked | ||
|---|---|---|---|---|---|---|
| 8 | 102 | COMMUNICATION, SCIENCE AND TECHNOLOGY | Communication | 29 June 2012 | ||
| Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri nina maswali mawili ya nyongeza. Kwanza katika Wilaya hii ya Manyoni na hasa hizo tarafa zilizotajwa za Kintinku na Nkonko tuliwasilisha kwa pomoja kwa upande mwingine wa Wilaya upande wa Magharibi tuliwasilisha maombi kwa Kata ya Mamaghembe Ipandye na Idondyandole. Sasa napenda kujua hali ya hizi Kata katika huo mchakato unaozungumza ikoje maana utafiti ulifanywa na imeonekana kabisa hawa watu kiuchumi wanaweza kupatiwa huduma hiyo? Swali la pili, ni kweli kwamba mwaka jana au mwaka juzi tulijaza fomu. Wakuu hawa wa Makampuni walikuwa kwenye Ukumbi wa Msekwa tukajaza fomu hizo lakini hali halisi inavyoonekana kwa kweli utoaji wa huduma hii ya minara unasuasua sana. Sasa napenda nieleweshwe ni nini hasa mahusiano haya? Ni ushawishi tu mahusiano kati ya Serikali na haya makampuni, uhusiano wake hasa ni upi katika kushawishi haya makampuni? Maana inaonekana kwa upande mwingine Serikali kama vile haina control kabisa katika eneo hili? |
||||||
| ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 102 SESSION # 8 | ||||||
|
||||||
| NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, kwanza nitakapoleta ile orodha tutatazama kama maeneo ya Jimbo lako yamo na kama hayamo basi utaongeza na tutayafanyia kazi. Kuhusu hili la pili, msingi wa biashara ya mawasiliano ni biashara ya faida na makampuni haya hayalazimishwi kupeleka mawasiliano katika maeneo ambayo wanaona hayana mvuto wa kibiashara. Ndiyo maana Serikali ilianzisha mfuko wa UCAF, Mfuko wa Mawasiliano kwa wote msingi wake ni kutoa ruzuku kwa makampuni ya simu kupeleka mawasiliano katika maeneo ambayo hayana mvuto wa kibiashara. Sasa mwanzo tulikuwa hatuna hakika kwamba moja, gharama halisi za kupeleka mawasiliano kwenye eneo mahususi ni kiasi gani. Kwa hiyo, ruzuku inayohitajika ni kiasi gani. Hizo taarifa hazikuwepo. Tulichofanya sasa hivi ni kufanya tathimini ya kila kijiji na kujua gharama halisi za kupeleka mawasiliano kwenye kila kijiji na kutangaza tender kwa kila kijiji mahususi na ambacho tunajaribu kufanya ni kwamba katika yale maeneo ambayo makampuni ya simu yana minara inayozunguka katika maeneo haya inawezekana kampuni ya Vodacom tayari imewekeza katika maeneo ambayo ni jirani na Manyoni magharibi na kampuni ya Airtel imewekeza katika maeneo jirani na Wilaya ya Liwale kwa hiyo tunajaribu kutoa ruzuku kulingana na uwepo wa Makampuni katika maeneo mahususi. Mheshimiwa Spika, tunaamini njia hii na utafiti tulioufanya upya na model hii mpya ambayo tumeitengeneza itasaidia kuharakisha zoezi hili na tayari tumepata fedha shilingi bilioni 45 kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya kugharamia awamu ya kwanza ya kazi hii. Kwa hiyo, nataka niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge kwamba baada ya kutengeneza utaratibu huu mpya zoezi hili litaenda haraka. Pale mwanzo tulikuwa tunachelewa kwa sababu tulikuwa hatuna hakika na kiwango cha ruzuku na utaratibu tuliouweka. Kwa hiyo, sasa hii sio ahadi tu. Hii sasa ni utekelezaji. |
||||||