You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Supplementary Question

mp Mpina, Luhaga Joelson[CCM]

Kisesa Constituency
Session No Question Number To the Ministry of Sector Date Asked
5 5 EDUCATION AND VOCATIONAL TRAINING Loans 8 November 2011
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa hivi sasa gharama za Vyuo Vikuu zimekuwa kubwa sana kwa maana ya ada na gharama zingine na kuwafanya wanafunzi wengi kukosa nafasi na uwezo wa kulipia gharama hizo. Kwa kuwa hapa nchini hivi sasa Vyuo Vikuu vya Serikali vimekuwa na gharama kubwa hata kuliko vile vya watu binafsi na kwamba hata hivyo Vyuo vya Serikali vinatoza ada tofauti kwa kila shule. Kwa mfano, Chuo Kikuu cha UDOM kinatoza degree ya sheria kwa shilingi 950,000 lakini Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kozi hiyo hiyo inatozwa shilingi 1,500,000.

Je, ni lini sasa Serikali itafanya utafiti huu wa kina wa kujua uhalali wa gharama ya kumsomesha Mtanzania ili gharama hizi zinazotozwa ziwe ndogo kiasi kwamba wananchi wetu wengi waweze kumudu gharama hizo?
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION #  5  SESSION #  5
mp Answer From Hon.Kawambwa, Dr. Shukuru Jumanne
EDUCATION AND VOCATIONAL TRAINING
WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO NA UFUNDI:

Mheshimiwa Spika, Serikali imelibaini hilo na imelitambua kwamba ni tatizo na katika juhudi za Serikali tayari kwa kushirikiana na Benki ya Dunia tumetoa katika mchakato wa kumpata Mtalaam Mshauri ambaye atatambua/atabaini students unit cost ama gharama halisi ya kumsomesha mwanafunzi katika Chuo Kikuu kwa program mbalimbali, mara tutakapoweza kupata students unit cost na mtaalam huyu tunategemea kumpata mwezi huu wa Novemba, mara tutakapopata hiyo itakuwa ni basis ya Serikali ya kuweza kutambua gharama ambazo Serikali ilipe kwa Vyuo lakini vyuo vinaweza vikatozwa kiasi gani kwa wanafunzi wake vile vya Serikali na vile ambavyo siyo vya Serikali.