| E-mail this to a friend | Printable version |
|
||||||
| Session No | Question Number | To the Ministry of | Sector | Date Asked | ||
|---|---|---|---|---|---|---|
| 8 | 146 | WATER | Water | 6 July 2012 | ||
| Mheshimiwa Spika, naomba nimshukuru sana Naibu Waziri kwa majibu yake mazuri, naomba kuuliza swali moja dogo la nyongeza. Mheshimiwa Spika mpango wa kuongeza vijiji au miji inayonufaika na maji ya ziwa Viktoria umekuwepo kwa muda mrefu na kwa miji midogo inayozunguka Mji wa Kahama, miji inayoguswa na mpango huo ni pamoja na Mji mdogo wa Kagongwa na Isaka na mpango huu umekuwepo tangu mwaka 2008 na mipango imekuwa ikiendelea. Nilitaka kufahamu. Je, Serikali imefikia hatua gani sasa katika mpango wa kuwapatia maji wananchi wa Isaka na Kagongwa Wilayani Kahama ambao wapo kwenye mpango wa maji ya Ziwa Victoria? |
||||||
| ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 146 SESSION # 8 | ||||||
|
||||||
| NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ni kweli kumekuwa na mpango wa kupeleka maji kwenye vijiji vilivyokuwa kandokando ya bomba linalotoa maji kutoka ziwa Victoria kwenda Kahama na Shinyanga na mpango huu umekuwa ukitekelezwa kwa awamu. Awamu ya kwanza ilikuwa ni kupeleka kwenye vijiji vilivyo kilomita tano kutoka umbali wa bomba ambavyo vilipatikana vijiji 54 na 39 vikaanza kupata maji. Awamu ya pili ikaongezwa vifikie vijiji 96 na uongezeke umbali wa kilomita 12 kutoka katikati ya bomba kila upande. Sasa hivi kinachofanywa ni kwamba tayari Serikali imeshatenga fedha katika awamu hii tunayokwenda kwenye Bajeti bilioni moja kwa ajili ya kufanya usanifu kwenye vile vijiji ambavyo vipo umbali wa kilomita 12, lakini vile vile kama utazingatia juzi tarehe 4 Julai, 2012 Wizara imeshatoa tangazo kwenye magazeti kuhusu zabuni ya kuepeleka maji Magu na Miji ya Ngudu na vile vile kutoka Victoria kwenda miji ya Meatu. Kwa hiyo, mipango inaendelea na tutaendelea kukamilisha awamu kwa awamu. |
||||||