| E-mail this to a friend | Printable version |
|
||||||
| Session No | Question Number | To the Ministry of | Sector | Date Asked | ||
|---|---|---|---|---|---|---|
| 8 | 106 | ENERGY AND MINERALS | Energy | 29 June 2012 | ||
| Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza. (a) Jambo hili la kupeleka umeme kutoka Makambako kuelekea Songea na Mbinga sasa hivi ni miaka karibu nane na ilikuwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya miaka mitano iliyopita. Sasa kwa kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga imetoa jenereta na liko tayari na imetoa kuanzia mwaka 2008, kuna ugumu gani wa REA kwenda pale na kufanya network ya umeme ili mji ule upate umeme? (b) Mheshimiwa Naibu Waziri anajibu tu hivi inaingia akilini au ama haiingii akilini kwamba makaa ya mawe yanachumwa pale Ngaka, yanapelekwa Malawi kuimarisha umeme wa Malawi na sisi pale hatuna umeme hivi inaingia akilini, ama haiingii akilini? |
||||||
| ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 106 SESSION # 8 | ||||||
|
||||||
| WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge na niwapongeze Madiwani wote wa Halmashauri ya Mbinga kwa kukubali na kuridhia kuachia jenereta moja ambayo ilikuwa ikitumika kwenye Kiwanda cha Kahawa itumike kupeleka umeme eneo la Mbamba Bay. Mheshimiwa Mbunge atakumbuka kuwa Mheshimiwa Rais ameweza kutoa jenereta mbili katika Wilaya ya Mbinga ili kutatua tatizo la umeme Wilaya ya Mbinga na ni kweli kabisa kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga imeweza kutoa jenereta iliyokuwepo kuipeleka Mbamba Bay, tayari tunafanya mazungumzo na nimekwisha iagiza TANESCO pamoja na REA watafute fedha kwa ajili ya kujenga miundo mbinu ya kusambaza umeme kwa wateja, kazi ambayo ingefanyika baadaye baada ya mradi wa kutoa umeme kutoka Makambako- Songea kwenda Mbinga Mbamba Bay ingekamilika. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge kupitia Halmashauri ya Mbinga wamekwenda hatua mbele zaidi ya kupata jenereta. Kwa hiyo, kazi yetu sisi ni kuhakikisha kwamba tunajenga miundombinu haraka ya kuwasambazia wananchi umeme. Mheshimiwa Spika, Katika swali lake la pili, jibu ni haiingii akilini. Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inatambua hilo na tunafanya kazi sasa hivi ya kuhakikisha kwamba rasilimali za makaa ya mawe zinatumika kwanza kutosheleza mahitaji ya umeme wa ndani kabla hatujafikia kuuza nje. Kwa hiyo, kwa hiyo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge makaa ya mawe yale hayapelekwi tu Malawi lakini pia viwanda vyetu vya Sementi vya Twiga, Mbeya pamoja na kiwanda cha Chai kinatumia makaa ya mawe haya yanayotoka Mbinga. Lakini pia tukijitosheleza kiu-meme, siyo vibaya pia kuuza kwa wenzetu. |
||||||