You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Supplementary Question

mp Arfi, Said Amour[CHADEMA]

Mpanda Mjini Constituency
Session No Question Number To the Ministry of Sector Date Asked
4 197 TRANSPORT Transport/Road 8 July 2011
Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Kwa kuwa, tatizo la usafiri katika Ziwa Tanganyika Serikali imekiri kupitia kauli na jibu la Mheshimiwa Naibu Waziri. Meli ya MV. Mwongozo imesimama toka mwaka 2008. Je, huku ndiko kujali matatizo ya wananchi kuchukua miaka mitatu meli haijatengenezwa?

ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION #  197  SESSION #  4
mp Answer From Hon.Mfutakamba, Athuman Rashid
TRANSPORT
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI:

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Said Amour Arfi Mbunge wa Mpanda Mjini kama majibu yangu ya nyongeza niliyoyatoa kwa maswali ya Mheshimiwa Kakosi.

Serikali inafanya upembuzi yakinifu na tumekwishapata mtaalamu wa kufanya feasibility study naomba tu awe na subira kwani hayo tutayakamilisha katika kipindi ambacho Serikali imeahidi kutatua matatizo hayo ya usafiri.