You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Supplementary Question

mp Arfi, Said Amour[CHADEMA]

Mpanda Mjini Constituency
Session No Question Number To the Ministry of Sector Date Asked
4 40 LANDS, HOUSING AND HUMAN SETTLEMENTS DEVELOPMENT Human Settlement/Land 14 June 2011
Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kupima na kuwa na Hati ni jambo moja, na dhamira ya kuwa na Hati ili ziweze kuwasaidia wakulima kupata mikopo na kuongeza tija kwenye kilimo. Serikali inatamka nini kuhusu taasisi za fedha kutokuheshimu Hati za kimila?
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION #  40  SESSION #  4
mp Answer From Hon.Ole-Medeye, Goodluck Joseph
LANDS, HOUSING AND HUMAN SETTLEMENTS DEVELOPMENT
NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI:

Mheshimiwa Spika, iko dhana kwamba Hatimiliki za kimila hazina hadhi sawa na Hati zitolewazo na chini ya Sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999. Napenda kurudia tena kama nilivyoeleza wakati nikijibu swali la Mheshimiwa Augustino Manyanda Masele, mwezi Aprili, kwamba kwa mujibu wa sheria, Hati za ardhi kimila zina hadhi sawa na Hati zitolewazo chini ya Sheria Na. 4 ya mwaka 1999.

Mheshimiwa Spika, naomba tu nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba wananchi wengi wa maeneo ambayo tayari wamekwishapata Hati hizi za kimila wamepata mikopo. Moja ya maeneo hayo ni Mbozi, wamepata mikopo. Juzi nilikuwa najulishwa kwamba wamefikia karibu shilingi bilioni 16 ya pembejeo na huduma zinginezo.

Mheshimiwa Spika, suala kubwa na hili ningependa nitoe maelekezo kwa Maafisa Ardhi wa Wilaya zote kwamba ni jukumu lao kuwaelimisha wananchi pamoja na kuhamasisha taasisi za fedha kutambua na kuheshimu Hati za Ardhi Kimila.

Mheshimiwa Spika, Hatimiliki za ardhi kimila, tofauti na Hati zinginezo, zenyewe bahati nzuri ni kwamba zina muda mrefu zaidi kuliko hati nyingine hizi.

Kwa hiyo, mimi nashangaa taasisi za fedha ambazo zitaacha kuheshimu Hati ambayo muda wake wala ukomo siyo kesho! Uhai mkubwa zaidi kuliko Hati zitolewazo chini ya Shertia Na. 4 ya mwaka 1999.
Kwa hiyo, ningeomba Waheshimiwa Wabunge wote tushirikiane kuhamasisha taasisi za fedha pamoja na kuhakikisha kwamba Maafisa Ardhi wanatimiza wajibu wao kwa kuwaelimisha wananchi umuhimu wa hati hizi. Nashukuru sana.