You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Supplementary Question

mp Arfi, Said Amour[CHADEMA]

Mpanda Mjini Constituency
Session No Question Number To the Ministry of Sector Date Asked
6 117 TRANSPORT Transport/Road 10 February 2012
Mheshimiwa Spika, Watanzania na hususan Wananchi wa Mpanda wameshachoshwa kabisa na hizi ngonjera zinazotolewa kama majibu ya Serikali.

(i) Kwa kipindi cha miaka sita ambayo nimekuwa Bungeni na kila mwaka nikiulizia suala la reli wametengeneza kilomita 33.9 katika umbali wa kilomita 210 kutoka Kaliua mpaka Mpanda kwa wastani wa kilomita tano kwa mwaka. Kwa maana hiyo, kilomita 210 ni miaka 40. Sasa ni lini kama swali lilivyoulizwa ambalo halijajibiwa; watakamilisha kazi hiyo?

(ii) Katika majibu aliyoyatoa Mheshimiwa Waziri ambayo hayamo katika maelezo aliyokuwa amenipa, ameeleza juu ya mabehewa na usafiri wa reli, lakini anasema kwamba tutahitaji sana upatikanaji wa fedha. Je, Watanzania wanaposikia kwamba mnajenga daraja la shilingi bilioni 300 na mkaacha kuiimarisha reli kweli mna utashi wa kuondoa matatizo katika nchi hii?

Ni Daraja la Kigamboni, bilioni 300 kwa ajili ya matajiri watakaojenga Mji wa Kigamboni.
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION #  117  SESSION #  6
mp Answer From Hon.Mfutakamba, Athuman Rashid
TRANSPORT
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI:

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Said Amour Arfi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwa muda mrefu tumejitahidi kuweka mipango ya kuiimarisha reli na ndiyo maana tukaingia hata mkataba na mwekezaji. Sasa haya yamekwisha, tupo katika mpangilio wa kuiboresha reli yetu wenyewe. Haya niliyomweleza Mheshimiwa Arfi ni mambo ya muda mfupi sana; ni mambo ambayo tutayatekeleza kwa muda mfupi iwezekanavyo.

Nimewaambia kuwa, kuna mataruma ambayo tunayatoa kutoka sehemu za Singida na sehemu za Tabora kuyapeleka kule kuimarisha ili Reli ya Kaliua - Mpanda ifikie uzito wa reli wa pauni 56 kwa yadi, lakini haya ni ya muda mfupi. Kama tulivyoeleza wakati wa kuwasilisha wakati wa bajeti yetu, kikubwa tunachotaka kukifanya sasa ni kubadilisha mfumo mzima wa reli zetu. Naomba watuamini hivyo; kwani tuna miaka minne bado ya kufanya kazi hiyo, tumeshapita kila mahali kukutana na wawekezaji ambao watatusaidia kufanya kazi hiyo, tupo katika mikakati ya mwisho ya kutafuta ni yupi ambaye tufanye naye kazi hiyo.

Naomba muwe wavumilivu mwone tutafanya nini baada ya miaka mine. Reli hii tunataka tuiboreshe itoke kwenye reli nyembamba tuliyonayo sasa hivi iende kwenye standard gauge ya mita 1.435, ambayo itaweza kwenda kuruhusu treni za speed kilomita 120 kwa saa zipite hapo na kuweza kuchukua mizigo mikubwa ambayo ipo Rwanda, Burundi na hapa Tanzania. Tunaelewa sisi Serikali kwamba, uchumi wa nchi hii unategemea sana ubora wa reli hii sambamba na bandari na hiyo, ndiyo kazi ambayo tunaifanya.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana.