| E-mail this to a friend | Printable version |
|
||||||
| Session No | Question Number | To the Ministry of | Sector | Date Asked | ||
|---|---|---|---|---|---|---|
| 10 | 111 | INFORMATION, CULTURE AND SPORTS | Information | 8 February 2013 | ||
| Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipatia nafasi ya kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza. Namshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri amekiri kwamba Serikali inatambua umuhimu wa watu wenye ulemavu wa kusikia na kuona kupata habari na kwamba Serikali imeshakamilisha na Kanuni na Sheria ya kuvitaka vyombo vya habari viwe na wakalimani kwa ajili ya watu hao wenye ulemavu. Sasa mimi ningependa kupata jibu kutoka kwa Waziri ni lini Serikali itupe timeframe ni lini watakamilisha Sheria hiyo ili iweze kutekelezeka na watu hao wenye ulemavu waweze kupata habari kama watu wengine? Swali la pili, kwa kuwa TBC ni Televisheni ya Taifa na inatumika kwa walipa kodi Watanzania pamoja na watu wenye ulemavu. Napenda kumwuliza Mheshimiwa Waziri haoni sasa ni wakati mwafaka sasa kwa kuanzia Televisheni ya Taifa iwe na wakalimani ili watu hawa waweze kupata habari? |
||||||
| ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 111 SESSION # 10 | ||||||
|
||||||
| NAIBU WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kama nilivyosema katika majibu yangu ya msingi ni kwamba tayari Sheria hii ya EPOCA Waziri mwenye dhamana ambaye ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ameshaisaini na amepeleka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa maana ya kuandikwa na kutoa kama tangazo ili zianze kutumika rasmi. Kwa hiyo ni wakati wowote kuanzia sasa Mwanasheria Mkuu anafanya kazi hiyo kwa maana ya kutekeleza kuandika GN ili zianze kutumika. Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli TBC ni chombo cha taifa na niseme kwamba moja ya matatizo makubwa ambayo yamefanya mpaka sasa kutokuwepo kwa wakalimani katika vipindi mbalimbali ni kutokana na gharama hizo za wakalimani. Lakini TBC inatoa nafasi kuna kipindi cha Wape Nafasi ambacho mlemavu ndiye huwa anasimamia kile kipindi. Mheshimiwa Mwenyekiti, tumepokea ushauri huo lakini pia kuanzishwa kwa Sheria hii na itakapoanza kutumika kila chombo cha habari kinapaswa kuwa na mkalimani wa alama za vidole. |
||||||