You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Supplementary Question

mp Genzabuke, Josephine Johnson[CCM]

Special Seat
Session No Question Number To the Ministry of Sector Date Asked
8 363 AGRICULTURE, FOOD SECURITY AND CO-OPERATIVES Food/Agriculture 13 August 2012
Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza.

Kwanza, kwa kuwa, wakulima wa Mkoa wa Kigoma hususani Wilaya za Kakonko, Kibondo na Kasulu, wakala wa Taifa Mbegu yaani Agricultural Seed Agency imewahamasisha kwa kupeleka mbegu ya Alizeti.

Je, Serikali sasa itawasaidiaje wakulima wa Alizeti kupata mashine za kukamua Alizeti kupitia mfuko wa pembejeo?

Pili, ili kuvutia uzalishaji wa Alizeti na mbegu nyingine za mafuta na kulinda viwanda vya ndani.

Je, Serikali itakuwa tayari kuzuia uagizaji wa mafuta ghafi kutoka nje?
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION #  363  SESSION #  8
mp Answer From Hon.Chiza, Eng. Christopher Kajoro
AGRICULTURE, FOOD SECURITY AND CO-OPERATIVES
WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA:

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Genzabuke kama ifuatavyo:-

Kama nilivyosema katika majibu yangu ya msingi, Wakala wa Mbegu yaani Agricultural Seed Agency tayati ameshaanza utaratibu wa kusambaza mbegu katika Mkoa mzima wa Kigoma na vikundi vingi vimeshajiandaa, vipo vikundi Kalege, Bulimanyi, Kabondo, Ruhita, Kalela, Nyachenda na kadhalika ni takribani vikundi 30.

Sasa tutakachofanya sisi ni kuvihamasisha vikundi ili viweze kupata mikopo kutoka katika mfuko wa Pembajeo. Mimi niko tayari kabisa kuvisaidia vikundi hivi na utaratibu huo utaanzia hukohuko ndani ya Wilaya zinazolima Alizeti, lakini lengo ni kuvisaidia ili viweze kupata mashine hizi ndogondogo na zinapatikana na hata Mkoani Kigoma kwenye maduka tayari mashine hizi zimeshafika.

Kuhusu kuvutia uwekezaji wa ndani hili swali nakumbuka liliulizwa na Wabunge wengi wakati Waziri wa Fedha akihitimisha hotuba yake na alisema kwamba kwa kweli kimsingi Serikali inakubaliana na kuweka ushuru ili kupunguza uingizaji wa mafuta kutoka nje ili angalau kuhamasisha uzalishaji wa mafuta ya ndani.

Lakini kama nakumbuka vizuri maelezo ya Waziri wa Fedha yalisema kwamba utaratibu huo sasa kwa sababu tupo katika makubaliano na wenzetu katika Afrika Mashariki na tupo tayari na makubaliano ya itifaki ya Ushuru wa Forodha, basi atawasiliana na wenzake katika Afrika Mashariki maana si rahisi kufika tu unazuia au unaweka ushuru mkubwa kabla hamjapatana na wenzenu katika Jumuiya. Lakini kimsingi nakumbuka Waziri wa Fedha alisema, hili limepokelewa na linafanyiwa kazi katika utaratibu huo.