| E-mail this to a friend | Printable version |
|
||||||
| Session No | Question Number | To the Ministry of | Sector | Date Asked | ||
|---|---|---|---|---|---|---|
| 5 | 106 | ENERGY AND MINERALS | Energy | 17 November 2011 | ||
| Mheshimiwa Spika, ninakushukuru. Kwanza kabisa, kwa niaba ya Wananchi wa Wilaya ya Kasulu na Wilaya ya Kibondo, ninapenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Serikali inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi, chini ya Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kwa kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi na kufunga umeme wa jenereta katika Wilaya mbili za Wilaya Kasulu na Kibondo. Baada ya shukurani zangu ni swali la nyongeza kama ifuatavyo:- Kwa kuwa kitendo cha kukamilisha Mradi wa Umeme katika Wilaya ya Kibondo na Kasulu kimeleta hamasa kubwa kwa Wananchi kutaka kuunganishiwa umeme tofauti na maombi ya awali; je, Serikali inawaahidi nini Wananchi wa Wilaya ya Kasulu na Wilaya ya Kibondo pamoja na Vitongoji vyake vikiwemo Vitongoji vya Mwilanvya na Murusi ambao wameomba lakini hawajaunganishiwa umeme? |
||||||
| ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 106 SESSION # 5 | ||||||
|
||||||
| NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nishati na Madini, ninapenda kujibu maswali ya Mheshimiwa Josephine Genzabuke, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, ninaomba uniruhusu nimshukuru kwa pongezi alizozitoa, kwa jitihada kubwa iliyofanyika kwa kupeleka umeme. Alikuwepo miaka mitano iliyopita na anajua kazi iliyofanywa na ukubwa wake. Kwa hiyo, ninaomba nipokee pongezi hizo kwa niaba ya Wizara na TANESCO. Mheshimiwa Spika, hili la Kibondo na Kasulu ni kweli kwa sasa umeme uliokuwepo kwa jenereta za Kibondo na umeme ulikuwepo kwa jenereta za Kasulu ni mwingi sana, kulingana na matumizi ya pale. Tatizo tulilolibaini ni kwamba, kwa sababu ahadi ilichelewa kidogo, watu wengi walishindwa kujiandaa kufanya taratibu za kuunganisha umeme. Kwa hiyo, kilichotokea ni kwamba, sasa hivi baada ya kuona umeme umekuja pale Kibondo na Kasulu, maombi yamekuwa mengi sana. Vilevile sasa pana jitihada za makusudi za kuunganisha kwa yale maeneo ya karibu. Kwa hiyo, hili jambo nimelipokea lakini ninamfahamisha Mheshimiwa Mbunge kuwa, kwa taarifa tuliyoipokea hivi sasa ni kwamba, REA wanajiandaa kutengeneza bill of quantities na kufanya tathmini ya jumla ya kujua kazi hizo mbili zitakwenda wapi pamoja na kupeleka umeme kuna eneo la Kabanga ambalo lilizungumzwa hivi karibuni nalo linafanyiwa kazi. |
||||||