| E-mail this to a friend | Printable version |
|
||||||
| Session No | Question Number | To the Ministry of | Sector | Date Asked | ||
|---|---|---|---|---|---|---|
| 5 | 103 | HOME AFFAIRS | Security | 17 November 2011 | ||
| Mheshimiwa Spika ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali moja la nyongeza. Kwa kuwa wapo madereva wazoefu ambao hapo awali walipatiwa leseni Daraja la C; na kwa kuwa kwa sasa walitakiwa kurudisha leseni hizo na badala yake wapatiwe Daraja D; je, Serikali haioni kwamba upo umuhimu wa kuandaa utaratibu mwingine kwa madereva ambao ni wazoefu na hapo awali walipatiwa Daraja C wanaporejeshewa leseni hizo wakaendelea kururejeshewa Daraja C ili kuondoa usumbufu kwa wale ambao kwa sasa wameshakuwa watu wazima hawawezi tena kumudu gharama za masomo? |
||||||
| ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 103 SESSION # 5 | ||||||
|
||||||
| NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, hili swali la watembea miguu nimelijibu; limeulizwa kwamba alama ziwekwe kule vijijini kwa sababu zipo mijini tu kwa waenda kwa miguu na waendesha baiskeli na kadhalika. Nikasema kwamba, inataka ushirikishwaji wa wengine wote na siyo mamlaka peke yake kuhakikisha kwamba hili linatendeka. Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la leseni, ninamwomba Mheshimiwa Mbunge jamani chonde chonde, hapa tunachokizungumzia ni uhai wa Watanzania na kumekuwa na mambo mawili yanajitokeza ndani ya Bunge hili. Jambo la kwanza ni lile la kusema kwamba, watu wahurumiwe wasipitie katika mambo ya mitihani kwa sababu ya suala la ajira. Hii ni ajira ambayo ni tofauti; hawa wanakwenda na roho za Watanzania mikononi mwao. Kwa hiyo, ninataka kusema kwamba, katika hili hakuna compromise, utaratibu uliowekwa utafuatwa, mitihani itafanywa, wale ambao wataonekana kweli wanastahili kupata leseni watapata, wale watakaoonekana hawastahili kupata leseni hawatapata. |
||||||