You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Supplementary Question

mp Kirigini, Rosemary Kasimbi[CCM]

Special Seat
Session No Question Number To the Ministry of Sector Date Asked
4 387 HOME AFFAIRS Security 9 August 2011
Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwa kuwa kanda hii maalum ya kipolisi ya Rorya na Tarime inao upungufu mkubwa sana wa vitendea kazi kama
magari na pikipiki, na kwa kuwa kanda hii ya kipolisi imeonyesha upungufu mkubwa sana wa utendaji wa kazi kutokana na upungufu wa vifaa hivyo: Je, Wizara ina mpango gani wa kuipatia kanda hii ya Tarime na Rorya vifaa kama magari na pikipiki ili waweze kutekeleza majukumu yao vizuri?
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION #  387  SESSION #  4
mp Answer From Hon.Kagasheki, Ambassador Khamis Juma Suedi
HOME AFFAIRS
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI:

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli tumekiri hata katika bajeti ambayo tumeitoa majuzi ni kwamba upo upungufu wa vitendea kazi na hii siyo katika maeneo ambayo ameyataja yeye, lakini pia yako maeneo mengi nchini ambayo Waheshimiwa Wabunge hapa wamekuwa wakiyazungumzia. Namhakikishia kwamba kadri tutakavyokuwa tunapata fedha na uwezo utakavyokuwa unaruhusu, ndivyo tutakavyokuwa
tunatoa vitendea kazi. Lakini kuhusu hali halisi ya Mkoa maalum huu wa Tarime - Rorya ni kwa
sababu ya matatizo yao. Tutajitahidi kadri tuwezavyo kuupa kipaumbele.