You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Supplementary Question

mp Khalifa, Khalifa Suleiman[CUF]

Gando Constituency
Session No Question Number To the Ministry of Sector Date Asked
4 10 HOME AFFAIRS Security 7 June 2011
Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa fursa ya kumwuliza Mheshimiwa Naibu Waziri, Alhaj Kagasheki swali moja. Pamoja na kazi nzuri wanayofanya Wizara ya Mambo ya Ndani kuwajengea askari nyumba, labda nizungumzie zaidi upande wa Zanzibar. Yale maeneo ambayo sasa hivi baadhi ya askari wengi wanaishi ni zile nyumba za zamani ni mbovu na zinatisha sana. Sasa pamoja na suala la kuwajengea nyumba mpya ambazo huwa ni mbili au tatu ambazo zinachukua familia 12 mpaka 15 si zaidi ya hivyo.

Je, wana mpango gani madhubuti wa kuboresha zile nyumba ambazo ni za zamani lakini zinakalika zikifanyiwa marekebisho ili kupunguza hii dhiki ya askari, kwa sababu unajenga nyumba mbili lakini wanaoingia ni kidogo tu?
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION #  10  SESSION #  4
mp Answer From Hon.Kagasheki, Ambassador Khamis Juma Suedi
HOME AFFAIRS
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI:

Mheshimiwa Spika, Mhesihmiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, alikuwepo Zanzibar na katika mazungumzo na katika kutazama hali halisi hili lilikuwa ni jambo ambalo limekuwepo.

Suala la maboresho pia zimo, yamo matatizo ya nyumba, ukarabati wa nyumba upande mmoja, lakini pia kujenga makazi mapya kwa askari kwa upande mwingine. Kwa vyovyote vile nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na nilihakikishie Bunge lako Tukufu kwmaba upande wa Serikali na upande wa Wizara azma tunayo na tunaona matatizo ambayo askari wetu wanakuwa nayo. Lakini kinachotukwaza hapa imekuwa ni suala la Bajeti.

Lakini nishukuru kwamba kumekuwepo na mazungumzo mazuri kati yetu sisi na Waziri wa Fedha lakini pia Kamati yako ambayo wewe ni Mjumbe kupitia Mwenyekiti wake mmekuwa mnafanya kazi kubwa katika kulisukuma hili na nina uhakika huko tunakokwenda siyo Zanzibar tu lakini pia Tanzania nzima tutaweza kuimarisha makazi ya askari wetu.