| E-mail this to a friend | Printable version |
|
||||||
| Session No | Question Number | To the Ministry of | Sector | Date Asked | ||
|---|---|---|---|---|---|---|
| 3 | 104 | HEALTH AND SOCIAL WELFARE | Health | 15 April 2011 | ||
| Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Nina maswali mawili madogo ya nyongeza. (i) Kwa kuwa tatizo hili linatokea zaidi katika kipindi cha mitihani. Je, Mheshimiwa Waziri anaweza kutueleza ni kwa nini inatokea katika kipindi cha mitihani? (ii) Kuna imani potofu zinazojengeka kwa wazazi na wazee wa vijiji kuwa ugonjwa huu ni wa kimazingara au mazingaombwe na wakati mwingine wanachinja mbuzi kutoa kafara na mambo mengine. Je, Mheshimiwa Waziri atawaeleza nini Wananchi au atatoa elimu gani kuhusu tatizo hili? Ahsante. |
||||||
| ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 104 SESSION # 3 | ||||||
|
||||||
| NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII: Mheshimiwa Spika, wanafunzi wengi huwa wanapata matatizo wakati wa mitihani. Wakati wa mitihani ndiyo wakati wanafunzi wanapata msongo wa akili mkubwa sana na unakuta kwamba, wakati mwingine wanafunzi hawa wanakuwa hawana mtu wa kuwashauri, hawana mtu wa kuwasikiliza na hawana uhakika kama kweli wataweza kufanya mtihani wakafaulu, wanaogopa wazazi wao watafanya nini nyumbani wakifeli na wanaogopa pia maisha yetu ya baadaye yanakuwaje kwa sababu ndicho kipindi kinachoamua kwamba, maisha ya mwanafunzi yanakuwaje baada ya ule mtihani. Kwa hiyo, ule msongo ndiyo unafanya wanafunzi wanakuwa katika extra stress, tunasema msongo wa kupita kiasi unajitokeza. Aidha, kwa kupata kifafa bandia au kwa kucheka au kwa kulia sana. Hiyo ni dalili kwamba, wanafunzi wana msongo mwingi. Mheshimiwa Spika, ninajibu swali la pili sasa; mara nyingi inapotokea hivyo, kwa sababu ni jambo ambalo limejitokeza hivi sasa, zamani tulikuwa na shule chache, tulikuwa na walimu wa kutosha, wanafunzi walikuwa wanafundishwa vizuri na walikuwa wanapata mahitaji yote yanayohitajika; ndugu zangu ninaomba niseme kwamba, wanafunzi sasa wanapata haya matatizo, wazazi hawakuzoea kuyaona, jamii haikuzoea kuona haya matatizo, yalikuwa yanatokea mara chache sana, shule zimekuwa nyingi, kwa hiyo yanaongezeka, kwa sababu hakuna maelekezo ndiyo sababu Wananchi wanaambatanisha na imani za kichawi. Hapa kwetu Tanzania na Afrika, ugonjwa wowote ule ambao hauna maelekezo na maelezo na ni mpya, mara nyingi tunatafuta sababu tunasema kuna mkono wa mtu na kutokana na hilo ndiyo maana Wananchi wanasema kwamba shule imerogwa. Ninaomba nitoe ushauri kwamba, wanafunzi wanapocheka au kulia na kuanguka ni maradhi ambayo yanaweza yakatibiwa na Daktari yeyote siyo uchawi, wala hakuna jirani anayeroga shule. Kwa hiyo, ninachoomba ni kwamba, wazazi wajaribu kuwatimizia watoto wao mahitaji yao. Walimu shuleni nao wawajibike kutoa huduma za ushauri nasaha kwa wanafunzi, kila shule iwe na mlezi wa wanafunzi hasa wanafunzi wa kike wa kuwasikiliza na huyo mtu awe tayari kuwasikiliza wanafunzi. Mara nyingi wanafunzi wanaweza wakamtaja ni nani ambaye wanamwamini, kwa hiyo, hakuna ushirikina ila ni matatizo ya ugonjwa wa akili ambao siyo mkubwa. |
||||||