You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Supplementary Question

mp Ndassa, Richard Mganga[CCM]

Sumve Constituency
Session No Question Number To the Ministry of Sector Date Asked
10 107 PRIME MINISTER'S OFFICE (POLICY, COORDINATION AND PARLIAMENTARY AFFAIRS) Central Government 8 February 2013
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa jicho lako kuniona.

Naomba nimwulize Mheshimiwa Waziri kwamba mbali na Mkoa wa Iringa unaojulikana kwa ulimaji wa Bangi ambao wanasema kwamba wao ni mboga kwao, ni mkoa gani mwingine unaoongoza kwa kulima Bangi?
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION #  107  SESSION #  10
mp Answer From Hon.Lukuvi, William Vangimembe
PRIME MINISTER'S OFFICE (POLICY, COORDINATION AND PARLIAMENTARY AFFAIRS)
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE:

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kumjibu Mheshimiwa Richard Ndassa swali lake la nyongeza kama ifuatavyo:-

Sijui kama ana mfano wa watu wanaofanana na Bangi watu wa Iringa huyu, lakini Iringa siyo Mkoa unaoongoza kwa kulima Bangi katika nchi hii. Mkoa wa Iringa siyo unaoongoza, Mkoa unaoongoza ni Mkoa wa Mara. Kwa hiyo, huo ndiyo Mkoa unaoongoza na hata ukiniambia nitoe takwimu hapa za Bangi tuliyoiteketekeza na kuikamata kwa kiasi kikubwa ni Mkoa huo wanaotoka akina Mheshimiwa Vincent Nyerere yaani Mkoa wa Mara.