Home » Members »Supplementary Question
Supplementary Question
 |
Murji, Hasnain Mohamed[CCM]
Mtwara Mjini Constituency |
|
|
|
|
|
|
| 4 |
183 |
WORKS |
Works |
5 July 2011 |
Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kuniona. Kwa kuwa, ahadi ya kivuko cha mto Pangani inafanana na ahadi ya kupewa kivuko cha kutoka Mtwara kwenda Msanga Mkuu.
Je, ni lini pia ahadi hii itatekelezwa?
|
| ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 183
SESSION # 4 |
 |
Answer From Hon.Mwakyembe, Dr. Harrison George
WORKS |
|
NAIBU WAZIRI WA UJENZI:
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Hasnain, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, sio tu kivuko cha Msanga Mkuu, lakini vile vile tuna kivuko cha Rusumo, kivuko cha Kilambo, vyote hivi mikataba ya kuleta vivuko hivyo tulisaini mwezi Juni, mwaka 2010 na ujenzi umeendelea vizuri na unakamilika wakati wowote katika kipindi cha mwaka huu na miradi hii yote iko kwenye Ilani ya Uchaguzi. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge ajjue kwamba tunaijali sana.
|
|
|
|