You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Supplementary Question

mp Ameir, Kheri Khatib[CCM]

Matemwe Constituency
Session No Question Number To the Ministry of Sector Date Asked
6 1 PRIME MINISTER'S OFFICE (POLICY, COORDINATION AND PARLIAMENTARY AFFAIRS) Central Government 31 January 2012
Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri. Watanzania tuna tabia, naweza kusema kwamba siku zote huwa tunasema tunaunda vyombo:-

(i) Katika jibu lako hili chombo hiki kitaundwa lini; lini tutakijua; na lini kitaanza kufanya kazi?

(ii) Mheshimiwa Rais wakati fulani alipotembelea Mikoa ya Kusini alitoa tamko kwamba kuna baadhi ya wanadini wanajishughulisha na masuala haya. Hili suala limefikia mahali gani na hawa watu wamechukuliwa hatua gani?
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION #  1  SESSION #  6
mp Answer From Hon.Lukuvi, William Vangimembe
PRIME MINISTER'S OFFICE (POLICY, COORDINATION AND PARLIAMENTARY AFFAIRS)
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, URATIBU NA BUNGE):

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Kheri Khatibu Ameir, Mbunge wa Matemwe, kama ifuatavyo:-

Tulipofanya semina hapa ya Waheshimiwa Wabunge, tulieleza umuhimu wa kuunda chombo kimoja chenye nguvu, kwa sababu shughuli hizi sasa zinashughulikiwa na vyombo vingi. Kwa mfano; Tume ya Kuratibu Shughuli za Dawa za Kulevya ipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Polisi pia wana Kitengo cha Dawa za Kulevya na idara mbalimbali nazo zinashughulikia masuala haya. Kwa hiyo, tunafikiri ni lazima kuwe na chombo kimoja ambacho kitakuwa na wataalam wote wanaohusika, ambao watakuwa na uwezo wa kukamata na kushtaki na kushughulikia wale vijana ambao wamepatwa na matatizo hayo kwa pamoja. Kwa hiyo, hicho chombo sasa hivi tumekitungia Sera na Sheria.

Nataka kumuahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba, vyombo hivi vyote na maandishi yote yameshafikia kwenye ngazi ya juu sana na ni nia yetu Serikali kwamba, tutaharakisha hili jambo ili liwe wazi. Tuligundua siku ile wakati wa semina kwamba hata sheria nyingine zinakinzana kiasi kwamba hata watoa haki hawatoi haki za msingi kulingana na makosa yalivyo. Kwa hiyo, ndiyo maana kuna umuhimu katika jambo hili, kurekebisha sheria, kutunga Sheria na Sera. Kwa hiyo, hilo jambo tunalifanya Juu ya Viongozi wa Dini; wakati wa Semina tulitoa mfano wa Kiongozi mmoja ambaye ameshakamatwa na kesi yake ipo Mahakamani, lakini vitendo hivi vimekuwa vinajitokeza tokeza na ndiyo maana Mheshimiwa Rais, alitoa rai wakati ule akiwa Mikoa ya Kusini. Wale wote ambao wamejihusisha na jambo hili, wawe ni Viongozi wa Dini, wafanyabiashara au watu wa kada zote, kesi zao ziko Mahakamani na wengine kesi zao zimeamriwa. Kuhusu hawa Viongozi wa Dini waliohusika, kesi zao ziko Mahakamani na siku ile wakati wa semina Waheshimiwa Wabunge, tuliwaonesha hata picha ya mhusika.