You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Supplementary Question

mp Daftari, Dr. Maua Abeid[CCM]

Special Seat
Session No Question Number To the Ministry of Sector Date Asked
10 10 WORKS Transport/Road 29 January 2013
Mheshimiwa Spika, namshukuru Waziri, kwa majibu yake, lakini nina swali dogo tu la nyongeza. Kwa kuwa hivi sasa mvua zimeanza Dodoma na baadhi ya nyumba zetu nyingi zinavuja. Ni ile ile kusema kwamba, TBA inapaswa kuwajali wateja wake, lakini hilo bado halijafanywa. Majumba yetu yote yanavuja, mapanya yapo ndani na board zote zinaloa zina mipaka na mito mbalimbali juu. Hata kule Kisasa kwa Waheshimiwa Wabunge wanakokaa, fancing haijatiwa.

Mheshimiwa Spika, je, Mheshimiwa Waziri ananiambiaje? Ni lini shughuli hii itashughulikiwa ipasavyo?

ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION #  10  SESSION #  10
mp Answer From Hon.Lwenge, Eng. Gerson Hosea Malangalila
WORKS
NAIBU WAZIRI WA UJENZI:

Mheshimiwa Spika, kwanza nakiri kwamba, kama nyumba zinavuja ni jukumu la TBA kuzifanyia matengenezo, kwa hiyo, kazi hiyo, tutakwenda kuishughulikia.

Mheshimiwa Spika, sehemu ya pili kuhusu uzio katika nyumba za Kisasa, hiyo, tumeiweka kwenye mpango; tutafanyia kazi na tutajenga uzio kwenye nyumba zile za kisasa.