Home » Members »Supplementary Question
Supplementary Question
 |
Chenge, Andrew John[CCM]
Bariadi Magharibi Constituency |
|
|
|
|
|
|
| 8 |
2 |
REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT |
Local Government |
12 June 2012 |
Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Kwa kuwa tatizo la uhaba mkubwa wa maji katika Mkoa wa Mpya wa Katavi linafanana sana na mahitaji makubwa ya maji katika Mkoa Mpya wa Simuyu hasa katika Makao Makuu ya Mkoa wa Bariadi. Je, Waziri anaweza akaliambia Bunge lako kwamba Serikali ina mpango gani wa muda mfupi na wa kati kukabiliana
na tatizo hilo la uhaba wa maji katika Mji wa Bariadi?
|
| ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 2
SESSION # 8 |
 |
Answer From Hon.Maghembe, Prof. Jumanne Abdallah
REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT |
|
WAZIRI WA MAJI:
Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa John Chenge, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, baada ya Mji wa Bariadi kutangazwa kama Mji Mkuu wa Mkoa wa Simuyu, Wizara yangu ilituma wataalam katika Mji huo kufanya tathmini ya mahitaji ya maji ya muda mfupi, wa kati na mrefu ili kuhakikisha kwamba Mradi wa Maji kwa ajili ya mahitaji ambayo yataongezeka unaweza kuanza kujengwa. Katika hatua ya kwanza, usanifu wa Mradi mzima unafanywa sasa na hatua zinachukuliwa kwa ajili ya upatikanaji wa maji katika muda mfupi. Ninapenda kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali imejiandaa vizuri kuupatia Mji huo maji salama.
|
|
|
|