You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Questions

Bwanamdogo, Saidi Ramadhani  [CCM]
Chalinze Constituency
Session No Question No To the Ministry of Sector Date Asked
4 274 FINANCE AND ECONOMIC AFFAIRS Higher Education 20 July 2011
Principal Question No
Mwaka 2009 Chuo cha Usimamizi IFM kilichukua eneo la kujenga chuo hicho katika vijiji cha Msata/Kihangaiko lakini hadi sasa ujenzi haujaanza:-

(a) Je, Serikali inatoa kauli gani juu ya suala hilo?

(b) Je, ni lini wananchi hao watalipwa fidia ya kuchukuliwa maeneo yao?
ANSWERS TO PRINCIPAL QUESTION #274 SESSION # 4
Answer From Hon. Silima, Pereira Ame
FINANCE AND ECONOMIC AFFAIRS
NAIBU WAZIRI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Fedha, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Said Ramadhani Bwanamdogo, Mbunge wa Chalinze, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

(a) Serikali bado ina nia thabiti ya kujenga Chuo cha Usimamizi wa Fedha katika Kijiji cha Msata na Kihangaiko. Ujenzi wa Chuo hiki unategemwa kufanywa kwa utaratibu wa PPP. Kazi zinazoendelea sasa ni upembuzi yakinifu na usanifu wa mradi ili kupata gharama za mradi na utafutaji wa wabia.

(b) Mheshimiwa Spika, napenda kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge na kulijulisha Bunge kwamba, wananchi wanaomiliki maeneo hayo watalipwa fidia katika mwaka huu wa fedha hatua kwa hatua kadri ambavyo uhakiki wa kuwatambua wahusika na stahili zao utakapokamilika.