You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Questions

Mukya, Joyce John  [CHADEMA]
Special Seat
Session No Question No To the Ministry of Sector Date Asked
8 260 HEALTH AND SOCIAL WELFARE Street Children/Orphans 25 July 2012
Principal Question No
Je, Serikali, inafanya uhakiki wowote wa
kuhakikisha ubora wa Vituo vya kulelea watoto yatima nchini vinavyoongezeka, ili kubaini kama vyote vinatekeleza malengo yaliyokusudiwa, badala ya waanzilishi wake kuvitumia kujinufaisha kupitia migongo ya watoto wenye shida?
ANSWERS TO PRINCIPAL QUESTION #260 SESSION # 8
Answer From Hon. Rashidi, Dr. Seif Seleman
HEALTH AND SOCIAL WELFARE
NAIBU WAZIRI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa
Afya na Ustawi wa Jamii, naomba kujibu swali la
Mheshimiwa Joyce John Mukya, Viti Maalum, kama
ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara, kwa kushirikiana
na wadau mbalimbali zikiwemo Wizara na Idara za
Serikali, Wadau wa Maendeleo na Taasisi binafasi,
imakuwa ikihakikisha kuwa watoto walio katika
mazingira hatarishi, wanapatiwa malezi, matunzo na
ulinzi kwa kuzingatia viwango vya ubora unaotakiwa.

Katika kusimamia Vituo vya Kulelea Watoto
Yatima, Wizara, inalo jukumu la kufanya usajili na
kuvipatia leseni vile vinavyokidhi matakwa, kwa mujibu wa Sheria. Kupokea na kuhakiki Taarifa za utekelezaji wa Vituo, ili kuona maendeleo ya watoto na Vituo kwa ujumla. Hadi sasa, vipi Vituo vya Kulelea watoto Yatima na walio katika mazingira hatarishi 98 vilivyosajiliwa
Kisheria na vinatoa huduma kwa watoto wapatao
3,958.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuhakikisha ubora
wa huduma zinazotolewa katika Vituo vya Kulelea
Watoto Yatima, Wizara, imeandaa Mwongozo wa
Uanzishaji na Usimamizi wa Vituo vya Kulelea Watoto walio katika mazingira hatarishi, wakiwemo yatima kwa mwaka 2006. Mwongozo wa Viwango vya Ubora wa Huduma za Malezi, Matunzo na Ulinzi kwa watoto walio katika Mazingira hatarishi kwa mwaka 2009.

Aidha, Wizara, imeandaa Kanuni kwa ajili, ya
utekelezaji wa Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009,
ambazo zinatarajiwa kukamilika hivi karibuni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na kuwepo
kwa ongezeko la Vituo vya Kulelea Watoto Yatima
hapa nchini, mwaka 2011 Wizara, kwa kushirikiana na Shirika la Kuhudumia Watoto (UNICEF), imefanya
tathmini ya makao ya watoto yatima na wanaoishi
katika mazingira hatarishi katika Mikoa yote ya
Tanzania Bara, ili kuona hali halisi ya huduma
zitolewazo kwa watoto katika makao hayo na iwapo
hazikidhi masharti, kwa mujibu wa Sheria.

Matokeo ya tathmini hiyo, yamesaidia kuweka
mikakati madhubuti ya kuboresha huduma katika
makao hayo, mikakati hiyo ni pamoja na kuhakikisha
Vituo vyote vinavyokidhi vigezo vipatiwe leseni na
uendeshaji kwa mujibu wa Sheria na visivyokidhi vigezo vifungwe. Kujenga uwezo kwa kutoa mafunzo kwa wamiliki na walezi wa vituo vya kulelea watoto yatima na Maafisa Ustawi, ngazi ya Halmashauri, kuhusu utoaji wa huduma zinazozingatia viwango vya ubora;
mkakati huo, utaanza kutekelezwa mwaka 2012/2013.