You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Questions

Session No Question No To the Ministry of Sector Date Asked
12 243 EDUCATION AND VOCATIONAL TRAINING Education 18 July 2008
Principal Question No
Kwa kuwa kilio kikubwa cha Walimu wa shule za msingi na za sekondari ni kucheleweshwa kupandishwa vyeo na kurekebishiwa mishahara yao baada ya kupandishwa daraja/vyeo:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kulitatua tatizo hilo?

ANSWERS TO PRINCIPAL QUESTION #243 SESSION # 12
Answer From Hon. Kabaka, Gaudentia Mugosi
EDUCATION AND VOCATIONAL TRAINING
NAIBU WAZIRI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Yono Stanley Kevela, Mbunge wa Njombe Magharibi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, mpango wa Serikali wa kutatua tatizo la kuchelewesha kupandishwa vyeo ni kuwapandisha walimu kwa mserereko Walimu wote waliokaa muda mrefu bila kupanda madaraja. Katika Sheria Na. 8 ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2002, Mamlaka ya kupandisha vyeo Walimu ni Idara ya Huduma kwa Walimu (TSD). Katika mwaka 2007/2008, kibali kilitolewa cha kupandisha jumla ya Walimu 38,000 wakiwemo 10,486 wa sekondari, vyuo vya ualimu na wakaguzi na walimu 27,514 shule za msingi waliokuwa hawajapanda madaraja kwa muda mrefu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara iliwasilisha (TSD) mapendekezo ya Walimu wa sekondari, vyuo vya ualimu na wakaguzi wa shule ambao tayari wamepandishwa madaraja na watumishi 6,230 wamerekebishiwa mishahara yao kulingana na vyeo walivyopewa. Aidha, Wizara inaendelea kurekebisha mishahara kadri barua za kupandishwa madaraja zinavyopokelewa.