You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Contributions

Abdulla, Amina Amour[CUF]

Special Seat
Session No Seating No Contribution Date Contribution To
4 4 14 June 2011 Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano, 2011/2012 – 2015/2016
Mheshimiwa Mwenyekiti, kufungu cha 27 kinachosomeka: “Serikali sekta ya umma ambapo kuwepo kwa utawala bora utawala wa sheria, demokrasia, haki za binadamu, kuzuia rushwa, uwazi na uwajibikaji ndiyo nguzo ya kufanikiwa kwa Mpango huu wa Maendeleo.” Lakini hivi vyote katika nchi yetu ni kikwazo, bado vinakosekana kwa sababu utawala bora haujafikiwa, kwani demokrasia ya kweli haijakuwepo, haki za binadamu zinakiukwa, rushwa inazidi kukua kila siku na uwazi na uwajibikaji haupo. Kwa hiyo, vyote hivi vinasababishwa na Katiba iliyopo ili kufanikiwa Mpango huu wa Maendeleo wa miaka mitano. Kwanza ni vyema kuwepo na Katiba mpya kwa sababu Katiba ndiyo inayosimamia Mpango huu wote wa Maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kifungu 28 ukurasa wa 21 unazungumzia umuhimu wa sekta binafsi katika maendeleo ya nchi. Sekta binafsi ndiyo inachangia kukua kwa uchumi, lakini Serikali haiipi umuhimu sekta binafsi, badala yake inawapa umuhimu wawekezaji kutoka nje. Ushauri wangu ni kwamba, kipaumbele kikubwa kipelekwe kwenye sekta binafsi na wawekezaji kutoka nje washirikiane na wazalendo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika ukurasa wa 23 kifungu cha 29 kinazungumzia kwamba, ili Mpango wa Maendekeo ufanikiwe, Serikali inatakiwa iwe na sera maalum ya fedha, kwa mfano, sasa hivi Taasisi zake kama Benki Kuu na mabenki mengine, fedha za kigeni kama dollar rate yake ni kubwa kuliko wanavyouza sekta binafsi. Kutokana na hali hiyo, watu wote hukimbilia kununua dola mitaani. Kwa hiyo, hakuwezi kuwa na sera bora ya kodi na fedha, na kwa hali hii, Mpango huu wa Maendeleo hauwezi kufikiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika ukurasa wa 25 kifungu cha 30 (d) kinazungumzia kwamba asilimia 60 ya nguvu kazi ya Taifa ni vijana. Lakini vijana wote wamehama vijijini na wako mjini, wanazurura mitaani na kufanya mambo maovu, kuvuta bangi, kujihusisha na madawa ya kulevya na wengine kuwa vibaka na wezi. Lakini tukirudi nyuma, chama chochote hakiwezi kupata ushindi ikiwa haijaungwa mkono na asilimia 60 ya vijana. Hawa vijana siyo kama tunakaa tukasema asiimia 60 ni vijana, bali tunawashawishi, tunawahamasisha, ndiyo hutuunga mkono na wakatupa kura. Kwa hiyo, sasa umefika wakati vyama vya siasa, CCM, CUF na CHADEMA na vyama vyote ambavyo vinashiriki kwenye uchaguzi, tuwahamasishe hawa vijana warudi vijijini na Serikali watengeneze mazingira mazuri ya kilimo kwa mfano, kuwakopesha pembejeo na zana za kisasa za kilimo na chama chochote kikishindwa kuwahamasisha hawa vijana kurudi vijijini wasiruhusiwe kushiriki kwenye uchaguzi wa mwaka 2015.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.