You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Contributions

Session No Seating No Contribution Date Contribution To
4 21 8 July 2011 Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2011/2012 Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)
Mheshimiwa Naibu Spika, Gases kama vile NO2. PM10, SO2 na kadhalika hutokana na muwako wa mafuta (liquid hydrocarbon) kwenye magari. Gases hizi husababisha uchafuzi wa hewa. Uchafuzi huu wa hali ya hewa husababisha magonjwa mengi kama vile pumu, nimonia, kansa za mapafu, magonjwa ya moyo (heart – rhythm problems etc) na kadhalika. Ninaamini uchafuzi wa hali ya hewa kwenye miji yetu mikuu kama vile Dar es Salaam, Mwanza na kadhalika, huongezeka siku hadi siku.

Mheshimiwa Naibu Spika naomba kufahamu: Je, kuma vipimo vya NO2, PM10, SO2 vinapimwa kila siku kwenye jiji la Dar es Salaam? Pia ninaomba kufahamu kiwango cha juu na cha chini cha air pollution katika Jiji la Dar es Salaam. Je, kuna adhari zozote ambazo zimeripotiwa kutokana na athari za air pollution katika jiji la Dar es Salaam?