You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Contributions

Kakoso, Moshi Selemani[CCM]

Mpanda Vijijini Constituency
Session No Seating No Contribution Date Contribution To
5 9 18 November 2011 Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa Mwaka 2011 (The Constitutional Review Act, 2011)
Mheshimiwa Spika, ninaomba nichukue fursa hii, nichangie Muswada huu wa Maandalizi ya Kuruhusu Katiba Mpya.

Mheshimiwa Spika, ninampongeza Mheshimiwa Rais, kwa ujasiri mkubwa wa kuanzisha mchakato huu wa Katiba inayowahusisha Wananchi moja kwa moja, kwa kuwapa nafasi ya kipekee waweze kutoa maoni yao juu ya mustakabali wa nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, huu ni wakati mwafaka wa kuruhusu Muswada huu ili uweze kujadiliwa, kwani ningependa tutoe kipaumbele juu ya Uzalendo wa Nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, pili, tuangalie juu ya kuendeleza historia ya nchi yetu kwa kutoubeza Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Mheshimiwa Spika, Muungano ni kwa manufaa ya Watanzania ambao tunaishi kwa kuthaminiana; Watanzania wanaoishi Zanzibar na wanaoishi Tanzania Bara, wote ni jamii moja. Hivyo, yeyote yule anayetaka kuupotosha Umma juu ya kuuvunja Muungano huu hatufai.
Jambo lingine ni juu maudhui ya Muswada ambao ameuwasilisha Mheshimiwa Waziri wa Katiba. Huu ni msingi wa mchakato wa kuunda Katiba Mpya, lakini kumekuwa na upotoshwaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani kuwapotosha Wananchi na kutafuta umaarufu sana juu ya ukweli uliowakilishwa na Mheshimiwa Waziri.

Mheshimiwa Spika, ningependa kuchangia kifungu cha 19, juu ya utaratibu wa kuwapata Wajumbe watakaounda Baraza la Katiba, uwe wazi na uhusishe watu wenye sifa maalumu na si vinginevyo. Tukifanya hivyo, tutakuwa tumewatendea haki juu ya kutokuwakilishwa vyema kwa Wananchi kama wenzetu wa Upinzani; siyo kweli kwani sisi Waheshimiwa Wabunge ndiyo tuliobeba dhamana na kutoa uwakilishi wa Wananchi ambao tumewawakilisha.

Mheshimiwa Spika, kuhusu wapi Ripoti itawakilishwa; mimi ninaamini mahali panapostahili ni kwa yule aliyepewa dhamana ya kuunda Katiba kwa mujibu wa taratibu za Katiba ya Nchi yetu, inayomtaka Mheshimiwa Rais aunde au kuteua Katiba hii.

Mheshimiwa Spika, kama wachangiaji wengi walivyochangia, mimi ninaunga mkono hoja hii.