| E-mail this to a friend | Printable version |
|
|||||
| Session No | Seating No | Contribution Date | Contribution To | ||
|---|---|---|---|---|---|
| 5 | 9 | 18 November 2011 | Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa Mwaka 2011 (The Constitutional Review Act, 2011) | ||
Mheshimiwa Spika, naanza kwa kuunga mkono Muswada 100% kwani kutokana na maendeleo ya kijamii kiuchumi na kisiasa kwa nchi yetu ni muhimu kuiangalia Katiba na kuiweka ilingane na mazingira ambayo tumefikia kwa sasa. Mheshimiwa Spika, naomba pia kusema kidogo juu ya wenzetu wa Chama cha CHADEMA kususia Muswada siyo sawa, wangeweza kutoa hayo mawazo yao Watanzania wangewasikia na pengine wangeyafanyia kazi, wamekosea sana. Mheshimiwa Spika, naanza na kuiangalia Ibara ya 5 katika Muswada inayosema Rais wa Jamhuri kushauriana na Rais wa Serikali ya Zanzibar kupata ushauri toka kwa Wanasheria Wakuu. Sijaona umuhimu wake pengine kwa mawazo yangu kuondolewa sioni sababu ya viongozi hawa kwenda kupata ushauri kwa Wanasheria. Suala la pili ni kuhusu Bunge la Katiba, chombo hiki kiwe ndio chombo cha mwisho kuhalalisha Katiba. Kinachowezekana ni kuongeza uwakilishi uwe mkubwa zaidi kwa makundi mbalimbali yanayojenga utaifa wetu na kama njia hii haitatumika basi lazima ipelekwe moja kwa moja kwa wananchi kupigiwa kura kwa msingi huu, hakuna sababu kupeleka rasimu kwenye vyombo viwili vikubwa na vitakavyotumia gharama kubwa sana lakini pia inaweza kuwa maeneo yanayoweza kuzua mgawanyiko ambao ungeepukwa. Mheshimiwa Spika, mwisho naunga mkono hoja hii. |
|||||