Contributions
 |
Mipata, Desderius John[CCM]
Nkasi Kusini Constituency |
|
| Session No |
Seating No |
Contribution Date |
Contribution To |
| 4 |
29 |
20 July 2011 |
Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2011/2012 Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi |
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Katika mchango wangu wa maandishi nilizungumzia juu ya mgawanyo wa rasilimali za Taifa kwa usawa na nikazungumzia juu ya mgawanyo wa masuala ya elimu kwamba Mkoa wa Rukwa ambao upo pembezoni hauna Chuo Kikuu chochote na wala Chuo cha ufundi, je, Serikali ina mpango gani ili kuuwezesha mkoa huu kupata Chuo Kikuu au Chuo cha Ufundi ukiachia kule Katavi ambako kuna Chuo cha VETA? Ahsante. |
|
|
| |