| E-mail this to a friend | Printable version |
|
|||||
| Session No | Seating No | Contribution Date | Contribution To | ||
|---|---|---|---|---|---|
| 5 | 9 | 18 November 2011 | Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa Mwaka 2011 (The Constitutional Review Act, 2011) | ||
Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja ya Mheshimiwa Celina O. Kombani, Mbunge, Waziri wa Katiba na Sheria kuhusu Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2011. Mheshimiwa Spika, Wananchi wa Igalula wote kwa ujumla wanaunga mkono hoja hii kupitia mwakilishi wao halali mimi. Hoja ya Upinzani haina mashiko kwani inalenga upotoshwaji wa Muswada huu kwa sababu zifuatazo:- Baada ya CHADEMA kushindwa Uchaguzi Mkuu 2010 na Igunga Oktoba, 2011 uchaguzi mdogo, sasa mjadala wa Katiba unaongozwa na Chama Tawala (CCM) badala ya CHADEMA, Mheshimiwa Rais Dokta Jakaya M. Kikwete, wao wanaona wateke nyara Muswada ili ndoto zao za mwaka 2015 kuingia Ikulu (haiwezekani) waweze kuanza mchakato wa kuunda Katiba mpya. Ubinafsi wa CHADEMA hautofanikiwa kwani Muswada huu utatoa fursa ya wananchi wengi ambao ni sauti ya Mungu. CHADEMA inawakilisha 14% ya Wabunge na kwa sababu wengi ni ndugu wa damu, uwakilishi wao ni mdogo. Hivyo Muswada utapita na baadae Katiba itapatikana. Precedence; Kenya, Uganda, Ghana na kwingine duniani utaratibu wa kupata Katiba mpya ni sahihi Tanzania kuufuata. Mchangiaji wa Kambi ya Upinzani CHADEMA anavunja Katiba kwa kuhoji Mamlaka ya Rais kama walivyofanya Desemba, 2010 kutoka nje ya Bunge Rais alipokuwa akihutubia. Tundu Lissu hana hoja bali ana matusi tu kwani ameona ajenda yao inashindwa wana lao jambo ovu. Mheshimiwa Spika, hawa wanaofadhili CHADEMA hawatutakii mema, wana wivu na amani na utulivu wetu. Tuwabaini na tuwaambie hawatafanikiwa kamwe. Tumethubutu, tumeweza na tunasonga mbele. Mheshimiwa Spika, Tume zimeundwa na Marais wastaafu Mzee Mwinyi (1991-Nyalali), Mzee Mkapa (1998 - Kisanga), leo Rais Dokta Jakaya Mrisho Kikwete ametoa fursa ya Muswada wa kurekebisha Katiba, CHADEMA wanang’aka, wana lao jambo. Wametumwa, tuwakatae. Baadhi ya ufadhili wamediriki kusema CCM imetawala kwa muda mrefu ipatikane njia ya kuiondoa madarakani. Wanadhani hii nia ya Muswada wa kuvuruga watafanya nchi isitawalike ili watwae madaraka. Hawatoweza kamwe hawa vibaraka CHADEMA. Mheshimiwa Spika, CHADEMA haina wawakilishi kule Zanzibar? Iweje hawataki Muungano? Hiki chama kweli ni cha familia isiyo na demokrasia! Balaa tupu. Ewe Mungu tuepushe na dhamana hii tuendelee na amani, mshikamano na utulivu. |
|||||