| E-mail this to a friend | Printable version |
|
|||||
| Session No | Seating No | Contribution Date | Contribution To | ||
|---|---|---|---|---|---|
| 4 | 17 | 1 July 2011 | Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2011/2012 - Ofisi ya Waziri Mkuu na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa | ||
Mheshimiwa Spika, naomba nichukue fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuchangia Hotuba hii, pili nachukua fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa Hotuba yake nzuri ambayo imejaa matumaini ya Watanzania. Mheshimiwa Spika, naomba nichangie upande wa kilimo, uchumi wowote katika nchi unategemea kilimo. Lakini katika mtazamo wa sekta ya kilimo katika nchi yetu bado hatujawekeza vizuri, naomba Wizara husika ijikite katika kilimo cha umwagiliaji. Kilimo cha kusubiri msimu wa mvua kimepitwa na wakati. Mheshimiwa Spika, nijikite katika sekta ya uwekezaji. Katika sekta hii ya uwekezaji na yenyewe bado hatujajipanga vizuri, wawekezaji ambao wanawekeza katika nchi yetu, wamekuwa wakijitajirisha kwa kuchukua madini yetu na kuondoka nayo. Naomba Serikali wapitie upya mikataba hiyo ili madini hayo yasipotee na tuweze kuyadhibiti ili tuweze kuingiza fedha za kigeni. Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. |
|||||